2017-04-19 16:15:00

Baba Mtakatifu kuwateua wajumbe maalumu kwenda katika matukio


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Kardinali Franc Rodé Rais Mstaafu wa Baraza la Kipapa kwa Mashirika ya Kitawa na vyama vya Kitume kuwa mjumbe maalumu katika maadhimisho ya miaka 550 ya kuanzishwa kwa Kanisa Kuu  kitaifa la Maria wa Scutari lijulikanalo  Mama wa Shauri jema huko Genazzano Mkoa wa Lazio nchini Italia. Maadhimisho ya kumbukumbu yatafanyika tarehe 26 Aprili 2017.

Alikadhalika;Baba Mtakatifu Francisko amemteua Kardinali João Braz de Aviz Rais wa Baraza la Kipapa wa maisha ya Kitawa, na Taasisi za  Maisha ya Kitawa kuwa mjumbe maalumu wa katika mkutano wa vyama vya kikristo duniania (VULTERIA ), utakao fanyika katika Kanisa Kuu la Mama Maria wa Fatima, kuanzia tarehe 4 hadi 6 Mei 2017 nchini Ureno.

Vilevile; Baba Mtakatifu Francisko amemteua Kardinali Paul Josef Cordes Rais Mstaafu wa Baraza la Kipapa linalo ratibu misaada ya Kanisa Katoliki kuwa mjumbe maalumu katika Ibada ya Mwaisho ya Kongamano la Maria huko Kazakhstan , itakayofanyika tarehe 13 Mei 2017 katika Kanisa Ku una Mama yetu wa Fatima Karaganda , ikiwa ni sambamba na mika 100 ya kutokea Mama Maria wa Fatima.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.