2017-04-15 15:22:00

Luxemburg: Ujumbe wa Pasaka 2017 kutoka Makanisa ya Kikristo


Katika dunia inayo endelea kutokuwa na uhakika, Wakristo waunganishe sauti zao kutangaza ushindi wa maisha dhidi ya kifo, na kutoa ushuhuda wa imani ya ufufuko. Ni ujumbe ulio andikwa na wawakilishi kumi na mmoja wa Baraza la Makanisa ya Kikristo  huko Luxemburg ikiwa ni ujumbe  Pasaka wa mwaka 2017.Ujumbe unaendelea kusema , Wakristo wajibidishe kujua vema na kuwa na utambuzi wa nguvu ya ufufuko wa Yesu katika kushiriki mateso yake.Pasaka ya mwaka huu kwa bahati nzuri inaadhimishwa  tarehe 16 kwa makanisa yote ye Kikristo. Ni tukio  linatokea mara chache sana kwa wakristo wote kufanya sikukuu ya Pasaka kwa pamoja, mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2014, ambapo tukio hili tena litafanyika mwaka 2025. Taarifa kutoka Gazeti la Sir linasema Baraza la Makanisa ya Kikristo huko Lussemburg wanapendelea kuonesha furaha yao na  kuishirikisha ujumbe wa Ufufuko wa Kristo kwa waamnini wote.

Aidha ujumbe unasema mada kuhusu tarehe ya Pasaka kwa makanisa yote ya Kikristo imekuwa jambo lenye utata kwa makanisa kwa muda mrefu, ambapo wameshindwa kupata ufumbuzi wa hilo.Lakini pamoja na hayo wakristo wote kila mmoja anakotokea, imani ya ufufuko ndiyo kisima cha furaha, matumaini na upendo. Kwa maana hiyo Ufufuko ni msingi wa Imani ya kila mkristo ni mwanga unao angaza.Viongozi hao wamesema "Tuko karibu kwa namna ya pekee katika sala zetu kwa ajili ya Wakristo wanaoteseka,na wasio kuwa na fursa ya  kuadhimisha Sikukuu ya ufufuko kwa uhuru na amani, maana hawa ni mwili wa mateso ya Yesu.

Ni ujumbe wa Pasaka kwa mwaka 2017 ulio sambazwa kwenye vyombo vya Habari kutoka katika Mabaraza  mawili ya Makanisa ya Kikristo Barani Ulaya na Uingereza kwa njia ya Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Ulaya Kardinali Angelo Bagnasco  na Askofu Christopher Hill wa  Kanisa la Ungereza na Rais wa Baraza la Makanisa ya Ulaya (Kek).Tuko karibu na nyinyi katika sala zetu , ndugu zetu wengi katika Kristo ambao wamekufa kwa ajili ya kutetea imaai yao, na kama  vile wale ambao wanaendelea kutoa ushuhuda, kwa kuheshimiana ,katika mazungumzo katika hali ya hatari na hivyo hawa ni mfano kwetu sisi. Viongozi wa dini hawa wa dini wanawaalika  wakristo wa Ulya kuwa na  ujasiri wa imani yao, na kushuhudia kwa furaha na uhakikauhakika wa upendo wa Mungu usio na kikomo.

Aidha viongozi hawa wanasisitiza wakristo wote kukaa karibu na wote wanao hitaji msaada bila kutazama utaifa, dini,kwa kusaidia  maskini, wagonjwa , wazee, mama na watoto, wafungwa , wahamiaji na wote ambao jamii imewatanga. Kusulibiwa ni hali halisi ya sasa maana  maisha ya binadamu kwa sasa ni kinyume na uumbaji ambao umeharibiwa vibaya sana kwa njia ya vita, uchoyo na dhuluma,na maisha  yanazidi kutishiwa na kuharibiwa.
Kwa walio  wengi  mara nyingi  kumekuwa na ishara za vurugu , na hofu, lakini Yesu Kristo ni mwenye nguvu kuliko milango yetu  iliyofungwa au kuta za mioyo yetu. Yeye alisema, “Amani iwe kwenu". Maaskofu wanaongeza  kuhusu  mgawanyiko uliopo kati ya wakristo na kuwaomba wajibidishe kwa hali zote  katika safari ya umoja , pia wanakaribisha  jumuiya zote za Kikristo kuwa chombo cha matumaini katika dunia inayoitwa kupatanisha na mwenyezi Mungu mwenyewe.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.