2017-04-12 15:58:00

Kuna ongezeko la Saratani kwa watoto wadogo wa umri 0 hadi 14!


Kiwango cha watoto wanaopata saratani kimeongezeka kutoka asilimia 13 kati ya mwaka 2001 hadi 2010, ukilinganishwa na miaka ya 1981. Ni taarifa ya  utafiti ulio chapishwa  12 Machi 2017 kwenye jarida la matibabu la Lancet .Ugonjwa huo uliofanyiwa  utafiti na taasisi ya kimataifa ya utafiti dhidi ya saratani, (IARC) matokeo yanaonesha kuwa watoto 140 kati ya watoto milioni moja wenye umri  tangu kuzaliwa hadi  14 wanapata saratani kila mwaka tofauti na miaka ya 80.Taasisi ya kimataifa ya utafiti dhidi ya saratani (IARC) ambayo ni tawi la shirika la afya ulimwenguni, (WHO) limetaja sababu ya ongezeko hilo kuwa ni pamoja na uwepo wa vifaa vya kisasa vya kubaini mapema saratani. Saratani ya damu ndiyo inaongoza kwa kukumba zaidi watoto ikifuatiwa na uvimbe kwenye mfumo fahamu.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo IARC Dkt. Christoper Wild amesema kichocheo cha saratani miongoni mwa watoto ni mfumo wa kijenetiki tofauti na inavyokuwa kwa watu wazima.Utafiti huo umedokeza kuwa pengine ongezeko hilo la watoto kuwa na saratani linaweza kuchochewa na kubadilika kwa uelewa wa madaktari kuhusu saratani kwa watoto au madhara ya vitu vya nje kama vile maambukizi au vichafuzi vya hali ya hewa. Takwimu za utafiti huo zilitoka katika masjala 153 za saratani katika nchi 62 ikihusisha asilimia 10 ya watoto wote ulimwenguni.

Sr Amgela Rwezaula 
Idhaa yak swahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.