2017-04-11 14:16:00

Mashine za kufua nguo kutolewa na Vatican kwa ajili ya masikini!


Baba Mtakatifu Francisko, ametoa zawadi ya Mashine ya kufua na kukausha nguo kwa ajili ya watu masikini na wasio  na makazi, na tangu tarehe 10 Aprili 2017 mashine hiyo  imeanza kufanya kazi rasmi. Hii ni huduma ambayo itatolewa  bure kwa ajili ya watu wote walio masikini na hasa zaidi wasio kuwa na makazi ambao wataweza kuosha nguo zao, kukausha na kunyosha mavazi hayo. Huduma hiyo ni sehemu mojawapo ya matendo ya huruma , ambayo Baba Mtakatifu mwenyewe amependa kuonesha matendo halisi na uzoefu wa neema.

Wakati wa kufunga mwaka wa Jubilei ya huruma,mojawapo ya ujumbe wa Waraka wa Kitume Jubilei ya Huruma, (Misercordia et misera) Huruma na Amani, kipengele cha matendo huruma kinaeleza ya kwamba ili kupata kuwa karibu na Kristo ni lazima kuanzia  ukaribu na jirani, kwa sababu hayo ndiyo mapenzi ya mungu na ndiyo ishara halisi ya huruma. Matendo halisi yanaundwa na matendo ya  nguvu katika  kutoa fursa ya huruma hasa kwa kijitoa maisha kwa wengine katika matendo mema ya neema. Kwa njia hiyo mashine ya kufua nguo ni ishara halisi ambayo imetolewa kutoka kwenye Mfuko wa  fedha wa masikini Vatican, ili kuonesha  kwa matendo halisi ya upendo , kama sehemu ya  matendo ya huruma ambayo inawarudishia adhi watu wengi wadahaifi na masikini ambao ni ndugu zetu, tunao itwa kwa pamoja kujenga mji tulio kabidhiwa. 

Sr Angela Rwezaula

Udhaa ya Kiswahili ya radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.