2017-04-10 14:40:00

Wakristo na Waislam wa Ninawi wanasema kuna haja ya amani duniani


Jumapili tarehe 9 Aprili 2017 Patriaki Louis Raphael Sako wa Kanisa la Wacaldei wa Babilonia anasema,matembezi ya mshikamano ya amani kwa ajili ya dini huko Ninawi  ni fursa ya matumaini kwa ajili ya Iraq na mchi zote Mashariki. Matembezi  hayo pia yanawashirikisha waislam na yameanzia katika mji wa Erbil yatamalizika baada ya wiki moja  katika Mji wa Alqosh.Mwandishi wa Habari wa Radio Vatican alihojiana na Patriki Sako juu ya matembezi haya, akasema ni kwa ajili ya amani  ili kuwaeleza watu ya kwamba kuna umuhimu wa amani. Ni matarajio yake watu kuitikia kwa nguvu zote katika kuanzisha arambee hiyo , maana wengi watapata fursa ya kutafakari na kufanya kuchanua mema na mabaya. Matembezi haya yata dumu kwa muda wa wiki moja yenye urefu wa kilometa 140Km.Itakuwa siku ya Jumamosi tarehe 14 Aprili 2017 huko Qaraqosh tayari kuadhimisha misa Takatifu ya mkesha wa Pasaka. 

Matembezi ya Mshikamano wa amani yanapitia katika sehemu ya ukanda wa  Ninawi mahali ambapo kuna mateso na yanaendelea kama vile huko Mosul na Iraq nzima. Wote kwa pamoja waislam kwa wakristo watakakutana kwasababu vijiji vyote hivyobado wanaishi  waislam wa kikurdi, waarabu na yazidi. Wanafanya matemebezi hayo kwa pamoja ili kuhamasisha umoja na kutaka kusema kwamaba vita, migogoro na utamaduni wa kifo inatosha.
Aidha Patriaki Sako, amesema Jumatano tarehe 12 Aprili 2017 atakwenda Erbil na Alhamisi Kuu ataadhimisha ibada Takatifu ya Misa katika kijiji cha wakristo ambapo atawaonsha baadhi ya wanakijiji miguu na baadaye  kula chakula pamoja .

Katika ujumbe wa Kwaresima 2017, Patriki Louis Raphael Sako wa Kanisa la Wacaldei wa Babilonia alitoa wito wa kufanya matendo ya huruma na makusanyo yalikuwa ni kwa ajili ya kusaidia watu wote bila ubaguzi. Na siku za hivi karibuni amekwenda Mosul, kwenye makambi mawili ya wakimbizi kwa ajili ya kuwapelekea chakula , madawa , maziwa ya watoto na familia 400,000. Wote walikuwa ni waislam ,hapakuwapo hata mkristo mmoja aliwaeleza kuwa, amefika kuwapa mshikamano,ukaribu na urafiki. Na katika mazungumzo yao na wakimbizi walisema, Mosul bila wakristo hawezi kutembea peke yao.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.