2017-04-09 17:03:00

Msalaba na Picha ya Mama Maria kila mahali viongeze amani na matumaini


Mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana , Baba Mtakatifu  ametoa salam kwa  mahujaji wote , na kwa namna ya pekee kwa walio udhulia Mkutano wa Kimataifa juu ya Sinodi ya Maaskofu na Maandalizi ya siku Vijana, ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la walei , Familia na Maisha kwa kushirikiana na Sekretarieti kuu ya Sinodi Maaskofu. Pia kuwasalimia vijana wote leo, ambao wamezunguka  maaskofu wao kusheherekea Siku Vijana katika kila Jimbo duniani. Hii ni hatua nyingine ya hija iliyo anzishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II ambapo mwaka jana wote vina wote wameunganikwa katika mji wa Cracovia , na sasa kualikwa  kwenda Panama Januari 2019.Kwa muda mfupi vijana kutoka Poland watawakabidhi msalaba wa Siku ya vijana Duniani kwa vijana wa Panama wanaojikita katika masuala ya kichungaji wakisindikizwa na viongozi wao wa Kanisa na Serikali .Tumwombe Bwana ili Msalaba na picha ya Mama Maria Mkuu , kwamba mahali popote itakapopita, imani na matumaini yaongezeke , na kuonesha upendo wa ushindi wa Kristo.

Baba Mtakatifu Francisko amesema  “Kristo ambaye anaingia katika mateso, na Bikira Maria tunawakabidhi waathirika katika mashambulizi ya kigaidi ya Ijumaa 7 Aprili 2017 huko Stockholm Sweden pamoja na wale ambao bado wamejaribiwa na vita, maafa ya ubinadamu. Aidha tuwaombee kwa Mungu waathirika ambao kwa bahati mbaya wameshambuliwa  Mjini Cairo asubuhi ya tarehe 9 Aprili 2017 katika Kanisa la Kikoptik”.
Baba Mtakatifu Francisko ametoa salam za rambirambi kwa Papa wa Kanisa la  Kikopta Tawadros II na kwa Taifa zima la Misri . Ameonesha masikitiko makubwa kwa majeruhi na waliopoteza maisha yao akiwaombea wapumzike kwa amani. Wakti huo wakiwatia moyo familia za ona kwamba yuko nao karibu kiroho.Ameongeza kusema,“Bwana aweze kubadili mioyo ya watu wanaopanda hofu na vurugu na kifo na pia mioyo ya wanao tengeneza na kusafirisha silaha”

Sr Anela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.