2017-04-09 15:24:00

Jamii inapaswa kuwalinda na kuwapokea jumuiya wa Waromania


Baba Mtakatifu amemtumia Barua Kardinali Peter Turkson Rais wa Baraza la Kipapa la Maendeleo ya  binadamu na wawakilishi wa  Mkutano katika Baraza hilo,  Barua iliyosainiwa na katibu Mkuu wa Vatican Pietro Parolin. Ujumbe umesema, Baba Mtakatifu amefurahishwa na kuutambua Mkutano wa tareh  7 Aprili 2017 , ulioandaliwa na Ubalozi wa Kipapa wa nchi ya Hungry kufanyika katika wa Vatican , ili kutafakari juu ya kushirikisha Waromania katika jamii pana ya Ulaya.

Vatican inawatia moyo wote wanao unganika kwa pamoja kufikiria njia nyingi ya kwamba jumuiya ya Waromani inatengwa bila kupata mafao ya kjamii, na ili kuweza kutafuta ufumbuzi wa kutoa vikwazo vinavyo zuia furaha na haki msingi za kutimiza wajibu wao. Barua hiyo pia inasema  “Iwapo watu  na jumuiya wako huru kushiriki kikamilifu katika maisha ya umma, na kutoa mchango wao, inawezekana kujenga amani ya kudumu, ambapo tamaduni na mila mbalimbali hulinda maadili yao, siyo kwa mitazamo ya kufunga bali kwa kupitia njia ya mazungumzo na ushirikiano” (Rej.Hotuba ya  Papa kwa hija ya Waromania tarehe 25 Oktoba 2015). 

Baba Mtakatifu anao uhakika kwamba watatimiza haya mawazo mema kwa njia ya dhamira nzuri  ya jamii yote ya kulinda usalama na kuwajali wale waliotengwa  ili kuweza kushiriki katika maisha ya jamii.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.