2017-04-09 12:56:00

Uso usio tamanika ndimo sauti inatoka ikiomba itazamwe na kupendwa!


Maadhimisho haya yana radha mbili, ya utamu na uchungu, ni furaha na mateso , kwa maana tunadhimisha Bwana akiwa anaingia Yerusalem, na kushangiliwa na mitume wake, kuwa ni mfalme, na maneo hayo pia yametamkwa katika simulizi la Injili ya mateso. Kwa njia hiyo mioyo yetu inajisikia mapambano , ni majaribu kwa  kiasi kidogo tu ambacho tunalazimika kusikia katika moyo wa Yesu siku ile ambayo watu na marafiki zake walilia Yerusalem.Ni sehemu ya maneno ya Mahubri ya Baba Mtakatifu Francisko wakati Kanisa Katoliki linaadhimisha Jumapili ya matawi Tarehe 9 Aprili 2017 . Misa Kuu ambayo imefanyika  katika uwanja wa Mtakatifu Petro na kuudhuliwa na maelfu ya waumini na wahujaji, wakiwemo vijana  wengi kutoka pande za dunia na hasa vijana wa Panama kwa ajili ya kupokea Msalaba Kutoka Cracovia Poland tayari kwa maandalizi ya Siku ya Vijana Duniani kwa mwaka2019.

Baba Mtakatifu francisko amesema;ni mwaka wa 32 ambao ni mwelekeo wa furaha ya Jumapili hii ambayo imekuwa na utajiri wa Sikukuu ya Vijana ;Siku ya vijana Duniani, ambayo kwa mwaka huu sherehe hiyo inafanyika  ngazi ya jimbo, lakini muda si mrefu uwanja huu utafaya uzoefu wa kusisimua, kutokana na upeo wazi wa tendo la kukabidhiana msalaba wa vijana, kati ya  vijana wa Cracovia na wale wa Panama.

Injili iliyosomwa inaelezea juu ya Yesu anayetelemka kutoka mlima wa mizeutuni, akiwa amepanda mwanapunda, ambaye hakuwa amepandwa na mtu, pia furaha kubwa ya mitume wake wanao msindikiza mwalimu kwa shangwe. Baba Mtakatifu amesema sherehe hii  ni kwa jinsi gani imeweza kuambukiza hata vijana wadogo na wakubwa wa mji kuungana na maandamano hayo wakipiga kelele za shangwe  wakati Yesu mwenyewe anatambua makaribisho hayo ya furaha, kwasababu ni nguvu isiyo weza kuzuilika kutokana na mapenzi ya Mungu, hadi wafarisayo kutoa manunguniko, yaliyo mfanya atoa jibu kwamba “kama hawa watabaki kimya, mawe yatapiga kelele.” » (Lc 19,40).

Kwa mujibu wa maandiko matakatifu hayataji kwamba tendo la kuingia namna hii katika mji mtakatifu alikuwa mtu mdanganyifu wa kueneza ndoto  za kinabii , au dini za kisasa au muuza moshi na mambo mengine.Yeye ni masiha kwa hakika na muonekano wake halisi, ni mtumishi wa Mungu na binadamu anaye kwenda kwenye mateso  na mwenye uvumilivu wa mateso makubwa ya binadamu.Kwa maana hiyo wakati tunafanya sikukuu ya Mfalme wetu tufikirie mateso ambayo atateseka kwa wiki hii. Tufikirie minong’ono , vitendo viovu, laumu,kutelekezwa, hukumu, kudhulumiwa , kupigwa viboko , taji la miiba na hatimaye tufikiriea njia ya msalaba, na kusulubiwa.

Aidha amesema Yesu alikuwa amewaeleza wazi wanafunzi wake” kama mtu yoyote anataka kuwa mfuasi wangu ni lazima ajikane nafsi yake , auchukue msalaba wake na kunifuata » (Mt 16,24).Yeye hakutoa ahadi ya heshima na mafanikio Injili inasema wazi, daima aliwajulisha njia gani ambayo angeweza kupitia , na kwamba ushindi  wake wa mwisho utakuwa ni kutoka katika mateso na msalaba. Kwa ajili ya kumfuasa Yesu, tuombe neema ya kufanya hivyo na siyo kwa maneno tu  bali kwa matendo , na kuwa na subira ya kubeba msalaba wetu na siyo kukataa,bali kumtazama yeye, kukubali na kuubeba siku hadi siku.

Baba Mtakatifu Francisko amesema ,Yesu aliyekubali kusulibiwa , hauombi tumtafakari katika picha au katika video zinazozunguka kwenye mitandoya kijamii. Hapana ;Yeye yupo katika wengi, kwa ndugu zetu wanaoteseka na masumbufu yake, wanaosumbuliwa katika kazi nguvu ya utumwa , katika matatizo mengi ya kifamilia , wanaosumbuliwa na magonjwa, wanaoteska kwajili ya vita na ugaidi, kwa sababu ya maslahi ya wengine wanotengeneza silaha na hizi zikatoa mashambulizi. Vilevile kwa ndugu wengi wanaodanganywa , wasio thaminiwa utu wao na kuondolea hadhi yao  kwasababu ni katika katika uso usio tamanika , ndimo sauti inatoka ikiomba zaidi itazamwe , itambuliwe na kupendwa.Amemaliza akisema , Siyo Yesu mwingine, ni yule aliye ingia Yerusalem kati ya wanao peperusha matawi ya mizeituni , ni yeye aliye bambwa kwa misumari msalabani na kufa katikati ya  majambazii.Hatuna Bwana mwingine badala yake :Ni Yesu mnyenyekevu mfalme wa haki, wa huruma na amani.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.