2017-04-08 15:42:00

Papa Francisko ateuwa Mabalozi wapya: Uingereza, Sweden na Iceland


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Edward Joseph Adams kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Uingereza. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Adams alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Ugiriki. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Adams alizaliwa tarehe 24 Agosti 1944 huko Philadelphia, nchini Marekani. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 16 Mei 1970. Kunako tarehe 23 Oktoba 1966 Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Askofu mkuu. Tangu wakati huo amefanya utume wake Bangladesh tangu mwaka 1966- 2002; Zimbabwe mwaka 2002 hadi mwaka 2007; Nchini Ufilippini tangu mwaka 2007- 2011 na tangu mwaka 2011 hadi mwaka 2017 alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Ugiriki hadi alipoteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Uingereza.

Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu James Patrick Green kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Sweden na Iceland. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Green alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini PerĂ¹. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu James Green alizaliwa kunako tarehe 30 Mei 1950 huko Philadelphia, nchini Marekani. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 15 Mei 1976 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto kunako tarehe 17 Agosti 2006 akamteuwa kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu tarehe 6 Septemba 2006. Akatumwa kama Balozi wa Vatican huko Afrika ya Kusini, Namibia na mwakilishi wa kitume Swaziland na Lesotho. Tarehe 15 Oktoba 2011 akateuliwa na Papa mstaafu Benedikto XVI kuwa Balozi wa Vatican nchini Ugiriki hadi mwaka 2017 alipoteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Sweden na Iceland.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.