Ni kuheshimu maisha kwa hali zozote na hasa kwa wale wadhaifu wasio kuwa na kuwa
na mtetezi , kwa mfano kuanzia hatua ya kutungwa kwa mimba,wazee, au walemavu, ni
wito wa nguvu uliotolewa na Askofu mkuu Bernadito Auza mwalikilishi wa Kudumu wa
Vatican katika Baraza la Umoja wa Mataifa hivi karibuni katika Mkutano wa Umoja wa
Mataifa mjini New York , mkutano ukiwa unahusu juu ya maendeleo endelevu na ongezeko
la watu.
Askofu Mkuu amesema, kwa miaka ya hivisasa kumekuwa mazungumzo kama vile bomu la ongezeko
la watu ambalo limepelekea baadhi ya serikali kufuata siasa kali ,zinazo unga mkono
juu ya uchunguzi wa watu, wakitafuta njia rahisi lakini inayohatarisha rasilimali
na kutokuendelea kwa nchi kama vile matumizi ya vidhibiti mimba kwa vizazi endelevu.
Askofu Mkuu anakubaliana nayo japokuwa anasisitiza ulazima wa kufikiria namna tofauti
katika kubainisha kanda na taifa.Inabidi kutofautisha watu katika nchi zitakazo edelea
kuongezeka watu kwa wakati imfupi na kwa upande mwingine ni lazima kutazama zile
ambazo hakuna ongezeko lolote , karibu ni sufuri , na wanafanya uzoefu kuona upungufu
wa idadi ya watu.Askofu Mkuu Auza amesema,kama ni kweli ya kwamba mgawanyo usio sawa
wa watu na rasilimali unaleta kizingiti cha maendeleo endelevu katika mazingira,
inabidi pia kutambua kwamba ongezeko la watu ni sawasawa kabisa na kushirikisha kwa
mali, katika jitihada za kuondoa umasikini, kutengeneza ajira na kutunza mazingira.
Mitindo ya kisasa ya kuzuia mimba siyo jibu amesema Askofu Mkuu Auza. Anayasema hayo
kutokana na kwamba nchi zinazoendelea idadi ya watu inapungua kwa kiasi kikubwa kwa
viwango vya kutisha,kutokana na sababu mojawapo kubwa ya matumizi ya vidhibiti vya
mimba na sababu nyinginezo nyingi za kisasa wanazo taka ziwe hata katika nchi zinazoendelea.Kwa
namna hiy askofu Mkuu anaongea kusema rasilimali za sayari hii zinatosha bali daima
zinatumika kwa namna isivyotakiwa , na bila kuwa na mgawanyo mzuri.Kwasababu katika
sehemu zilizoendelea , kuna hata matumizi makubwa , na wakati huo matumizi ni madogo
katika ngazi ya umasikini, vilevile ndiyo wahusika katika masoko kwani wanazuia nchi
masikini kuingia katika masoko ya nchi tajiri, katika mgawanyiko wa rasilimali na
katika uharibifu wa mazingira.
Katika nchi zinazoendelea, kinyume ni kwamba zinazidi kuongezeka ukosefu wa haki
na umasikini ambao unasababishwa na rushwa ,vurugu za kivita , na maafa mengineya
asili lakini yaliyosababishwa na binadamu ambaye uzuia kukua kwa afya njema ya watu.
Askofu Mkuu Auza anatoa ushauri katika kutoa jibu juu ya suala hili muhimu kuelekeza
mambo matatu tatu, ya kwanza ikiwa ni mshikamano, amani na usalama. Hiyo inahitaji
mabadiliko ya kisiasa, kikazi, kijamii, huduma, kwa pande zote mbili ikiwa katika
nchi zilizoendelea na zile zinazoendelea.Inahitajika mkakati wa maendeleo endelevu
yanayo mtazama mwanadamu na utu wake kwa ujumla,kuanzia wale walio baguliwa na kwa
kuwashirikisha wote siyo katika vigezo vya uzalishaji au kutokuzalisha, bali kuanzia
na thamani ya kila mtu awe kijana au mzee.
Anaongeza akisema hakuna yoyote anayepaswa kuachwa nyumba kwasababu wote tunapaswa
kushrikishana mizigo yetu.Lakini anaonya kwamba nchi masikini zisiendelee kutoa misaada
ya masharti kwa ajili ya vidhibiti mimba.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |