2017-04-07 16:55:00

Sote tumehesabiwa wenye haki katika imani ya Kristo Bwana Yesu


Padre Raniero Cantalamessa mhubiri wa nyumba ya kipapa katika  mahubiri yake ya tano ya Kipindi cha kwaresima tarehe 7 Aprili 2017, yenye kuongozwa na kauli mbiu  “Hawezi mtu kusema Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu”. (Rej. 1 Kor. 12: 3), amechambua Barua ya Mtakatifu Paulo kwa Warumi isemayo juu ya kuhesabiwa wenye haki (Reg.Rm 3, 21-28). Na hasa tafakari lake limetazama kwa undani juu ya mwanzo wa mageuzi ya Kanisa la Waluteri. Cantalamesa ameuliza je ni kitu gani kilisababisha uwepo wa utangano kati ya Kanisa na Ulaya mahali ambapo ndiyo kiini cha dini ambapo hata leo katika baadhi ya  waamini wa makanisa  na baadhi ya nchi za Ulaya mashariki , mafundisho ya utangano kati ya wakatoliki na waangilikani bado hujitokeza kwa kiasi fulani.

Lakini Roho Mtakatifu tuliye mtazama katika tafakari zilizopita, anatupeleka katika ukamilisho wa ukweli wa Yesu mwenyewe hasa zaidi katika maajabu ya Pasaka. Roho huyo anatuangaza kwa mantiki sahihi ya imani yetu katika Kristo yaani namna ambayo ukombozi unatendeka hadi kutufikia leo hii ndaniKanisa.Ametafakari  kwa kirefu mwanzo wa mageuzi ya Kanisa la kiluteri na hasa mawazo ya Luther juu ya kuhesabiwa imani kwa kutambua kwamba  mageuzi hayo ya Kidini yaliyochochewa na watu kama vile yeye mwenyewe Luther, Calvin, na Zwingli, yaliyosababisha kuundwa kwa dini mpya inayoitwa Uprotestanti. Kuhesabiwa kuwa mwenye haki kupitia imani ndilo fundisho kuu ambalo Luther aliacha katika Uprotestanti. Maeneo ya Ujerumani yaliyotawaliwa na wakuu yaliunga mkono imani ya Kiprotestanti au ya Kikatoliki. Uprotestanti ulienea na kuungwa mkono na watu wengi huko Skandinavia, Uswisi, Uingereza, na Uholanzi. Na leo dini hiyo ina wafuasi wengi sana pamoja na kwamba imeenea duniani kote.

Kuhesabiwa wenye haki :ni mafundisho ya Paulo au ya Yesu?.

Kwamba tatizo linatokana na Yesu kwamba hakuwa amesema jambo lolote kuhusiana na hilo. Lakini mafundisho ya Mungu  yanayokubaliwa na watu kuwa waadilifu  hayakuundwa na Paulo, bali ndiyo kiini cha ujumbe wa Injili , ni Yesu mwenyewe ,ni kwa njia  zozote zile  ambazo mtume alizitambua ili kutaka  kuonesha moja kwa moja juu ya  mfufuka au kwa ajili ya mapokeo ambayo yeye mwenyewe amesema kupokea na ambayo kwa dhati ni maandiko yake kuwa “ mimi niliwakabidhi nyinyi mambo muhimu sana ambayo mimi niliyapokea, kwamba Kristo alikufa kwa ajili yetu na kufuatana na maandiko matakatifu” (1Kor 15, 3), kwa njia hiyo ni kuthibitisha kwamba nwanzilishi wa ukristo ni Yesu mwenyewe na wala siyo Paulo.

Kiini cha mafundisho yanatokana na neno la Injili  yaani habari njema , ambayo kwa hakika Paulo hakuunda mafundisho hayo kutokana na bure, kwasababu yana msingi na kiini chake. Mwanzo wa utume wake Yesu alikwenda akitangaza muda umekwesha, ufalme wa Mungu uko karibu , tubuni na kuamini Injili.( Mk 1,15). Je inawezekanaje kutangaza hili na kutoa habari njema , iwapo wito huo  ni hatari wa kubadilisha maisha? Yaani ule ambao Yesu mwenyewe anatamka kwamba ni ufalma  wa mbingu ambao ndiyo mwanzo wa ukombozi wa Mungu  katika kujitoa kwa binadamu . Mtakatifu Paulo ana anaita haki ya Mungu , lakini ndiyo ukweli hali wa ufalme  wa Mungu na haki ya Mungu ni  vitu viwili vinavyokwenda sambamba , kutokana na maneno yake mwenye Yesu aliyo sema tafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake (Mt 6,23).

Yesu alipokuwa akisema kwamba tubuni na kuamini Injilia alikuwa akifundisha tayari kukubali haki wakati wa imani. Kabla ya ujio wake, kutubu maana yake ulikuwa  ni kurudi nyuma, kama inavyo onesha kwenye neno la kiyahudi Shub;maana yake kurudi katika agano la sheria kwa upya iliyovunjika. Kutubu pia kuna maana nyingine msingi katika utauwa, kimaadili, maridhiano , na hasa katika kubadili mwendendo wa maisha. Kubadilika ni hali inayoruhusu ukombozi, kwa maana tubuni na mtaokoka. Maana yake Kutubu na uokovu vinawajia ninyi. Na  ndiyo maana ya kutubu hadi kufikia enzi za Yohane Mtabatizaji. Kutoka katika  kinywa cha Yesu maana hiyo kimaadili, ilikuwa katika ngazi ya pili na hasa wakati yeye anaanza utume wake, kulinganisha na maana mpya aliyoanza Bwana Yesu .Kwa maana hiyo kutubu na kubadili haina maana ya kurudi nyuma kwa kutii sheria za kizamani, badala yake ni kupiga hatua mbele na  kuingia katika  agano jipya , ili kukaribia ufalme huo uliojitokeza  na kuingia ndani yake, lakini ni kuingia kwa  njia ya imani .

Tubuni na kuamini siyo  vitu viwili tofauti  bali ni kutambua mambo mapya  na  kufikiria kwa namna mpya. Maandishi mengi kutoka katika ni Injili inaonesha na kuthibitisha tafsiri hiyo. Mojawapo ni ile ambayo Yesu mwenyewe alisisitizia juu ya umuhimu wa kuwa kama watoto wadogo ili kuingia katika ufalme wa mbingu.Tabia ya mtoto ni kwamba hana lolote la kutoa , bali anaweza tu kupokea, yeye aombi lolota kwa wazazi wake kwasababu tayari amefanyia kazi kwani yeye anajua tu kupenda na kupokea bure.Padre Cantalamessa ameelezea juu ya matatizo yanayo jitokeza katika kutafsri namna ya kuokoka akitazama kipindi cha Yesu, akiwa na wandishi, mafarisayo na walimu wa sheria, ambapo Yesu aliwambia amini huyu mtoza ushuru alirudi nyumbani akiwa amesamehewa, maana kila anayejikweza atashushwa na kila anayejishusha atakwezwa.

Je, ni namna gani ya kutangaza haki kwa ajili ya imani?
Tunaweza kuhitimisha nini kwa kutazama juu ya miongo mitano ya mageuzi ya kiluteri?Padre Cantalamessa anatoa ushauri kwamba miaka hii ya mageuzi isiweze kuwa tasa kwa kushikiria tu yaliyopita, katika kutafuta makosa na sababu zisizo na msingi, na ambazo zimepita. Inalazimaka kupiga hatua mbele , kama mto ufikapo sehemu fulani umefungiwa uendelea kujaa hadi juu mwisho kupata mkondo wa kuendelea na njia nyingine.Hali kwa sasa imebadilika iliyosababisha mageuzi hayo hadi kufikia  kutengana na Kanisa la Roma .Kwa maana hiyo tatizo  namba moja ambalo ambalo Luther alikuwa nalo yaani  jinsi gani ya kuondoa dhambi katika nafsi ili kupokea msamaha wa dhambi; kwasasa tatizo hilo hakuna kwani ni kinyume maana sasa ni kujibidisha kwa jinsi gani ya kufundisha mtu  aliyechanganyikiwa kila kitu ili aweze kutambua nini maana ya dhambi.

Hiyo haina maana ya kutojali utajiri wa mageuzi yaliyofanyika , au kutamani kurudi nyuma kwa yote yaliyopita. Badala yake ni kuruhusu wakristo wote kufaidika mengi na muhimu  ya  mafanikio kwa mara nyingine tena baadaya ya  uhuru kutokana na upotofu fulani katika hali iliyojitokeza na kuweza kuiweka katika msingi wake. Haki ya imani katika Kristo inatakiwa kutangazwa leo katika Kanisa lote kwa nguvu zaidi kuliko. Hata hivyo katika upinzani ambao unatajwa katika matendo ya Agano Jipya lakini tofauti ya madai ya mtu wa kisasa anayetaka kujikoa na sayansi yake ya teknolijia au katika aina nyingine za kiroho za kubuni kwamba zinatuliza; Hizi ndizo kazi za mtu wa kisasa anazo amini.

Padre Cantalamessa amesema kwamba, anaamini kama leo hii Luther angerudi katika maisha , ndiyo njia ambayo yeye angeweza kuhubiri leo hii juu ya kuhesabiwa haki kwa imani. Aidha amegusia juu ya Tamko la mwaka 1999 wa mkataba wa maafikiano, ambao Kanisa la Kiangiliani na Katoli walikubalina ambao amesema unatoa utambuzi wa kweli na kwamba ni msingi kipengele kisemacho  ”Maafikiano yetu juu ya kweli kadhaa za msingi ya mafundisho ya kuhesabiwa haki lazima yawe na uwezo wa kujikita katika maisha na ufundishaji wa Makanisa yetu, na kuthibitika katika hayo. Lakini bado kuna masuala yenye umuhimu wa viwango mbalimbali yanayohitaji kubainishwa zaidi, ikiwa ni pamoja na uhusiano wa Neno la Mungu na mafundisho ya Kanisa, eklesiolojia (elimu juu ya Kanisa), mamlaka katika Kanisa, umoja wa Kanisa, huduma, Sakramenti, uhusiano wa kuhesabiwa haki na maadili ya kijamii. Twaamini kwamba maafikiano tuliyoyapata ni msingi imara kwa ajili ya ubainifu huo. Makanisa ya Kilutheri na Kanisa Katoliki la Roma yataendelea kujitahidi pamoja ili ufahamu huu wa pamoja wa kuhesabiwa haki uzidi kukua na kuzaa matunda katika maisha na ufundishaji wa Makanisa .(Rej. n 43).

Kwa njia hiyo hatupaswi kupoteza mtazamo wa Mtume Paulo juu ya kuhesabiwa haki , kwasababu ni kweli kwamba tumehesabiwa haki kwa ajili ya imani katika Kristo , na siyo kwa ajili ya neema tu, pia ni kwa ajili ya neema ya Kristo. Kristo ni moyo wa Ujumbe , kabla ya neema na Imani. Ni yeye leo kama Kanisa , kama binafsi na siyo mafundisho.Ni lazima kufurahi kwasababu hiki ndicho kinachoendelea katika kanisa na kwa kiasi kikibwa kuliko kawaida tulivyo zoea kufikiria.Amesema kwa miezi miwili ya karibuni amwezeza kushriki mikutano miwili , mmoja Uswisi, uliyo andaliwa na makanisa ya Kiluteri na wakatoliki, mwingine Ujermani , ulio andalia na Wakatoliki, na kushiriki Waanglikani. Na huo wa mwisho amesema kwamaba ni kama ishara ya nyakati.Kulikwa na wakatoliki 6000 waliteri 2000 wengi wao wakiwa vijana kutoka Ujermani.

Kutokana na kwamba Padre Cantalamesaa alikuwa ni mmojawapo wa kutoa hotuba, aliomba kama angeweza kuongelea juu ya umoja wa wakristona wahusika, wakamjibu kwamba wanatamani kuishi umoja badala ya kuongelea juu ya umoja. Na hivyo Cantalesaa amemalizia akisema walikuwa halali kusema hivyo kwasababu hizo ndizo  ishara na maelekezo ya roho ya Baba Mtakatifu Franciskoanayotaka tuendeleze. Heri na Sikukuu ya Pasaka.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.