2017-04-06 16:33:00

Vijana tambueni kuwa siku ya vijana ni matumaini ya dunia mpya


Mkutano wa maandalizi ya siku ya Vijana Pana umeanza tarehe 5 Aprili 2017  mjini Vatican ulio andaliwa na Baraza la Kipapa kwa ajili ya Walei  , familia na Maisha , wenye kauli mbiu kutoka Cracovia kwenda Panama, sonodi njiani na vijana. Ni vijana kutoka nchi mia moja duniani: Hawa ni kutoka katika mabaraza ya maaskofu wa Afrika ya kusini na Kaskazini, wakiwa 104 , na wawakilishi wa nchi 44, wa  mashirika , makundi, vyama vya kimataifa ya vijana Katoliki. Lengo la Mkutano huo ni kukabiliana na mada ya siku ya Vijana dunia iliyofanyika Cracovia Poland na itakayofanyika Panama mwaka 2019. Mkutano huo unatazamia kualizika na tarehe 9 Jumapili wakati vijana wa Cracovia watakabidhi msalaba na picha ya mama Maria kwa vijana wa Panama kwaajili ya maandalizi ya Siku ya Vijana Duniani.

Kama kawaida ya makabidhiano hayo yatafanyika wakati wa  maadhimisho ya Misa takatifu ambayo ni Jumapili ya matawi, itakayoadhimishwa na Baba Mtakatifu Francisko saa nne asubuhi katika uwanja wa Mtakatifu Petro .Wawakilishi kutoka Panama wataongozwa na Askofu Muu wa Panama Jose Domingo Ulloa Mendieta, Askofu Jose Luis Lacunza wa Jimbo la David Askfo Rafael Valdivieso wa Jimbo la Chitre na Askofu msaidizi wa Panama Uriah Ashley. Mkutano umegawanyika katika sehemu ya kazi vingele tofauti tarehe 6 na 7 watatazama Sinodi ya Maaskofu inayotazamiwa kufanyika Oktoba 2018 katika mada ya Vijana imani  na utambuzi wa miito, na pia familia na maisha . Jumamosi tarehe 8 Aprili 2017 mkutano wa wawakilishi wa Huduma ya kichugaji ya vijana kutoka duniani kote wataweza kujulishwa kwa ufupi maandalizi ya siku ya Vijana ya panama, Askofu Mkuu wa Panama atawakilisha sehemu mbalimbali muhumu hasa aina za matukio , matarajio ya kichungaji na maandalizi , na pia kuonesha wahusika wa Kamati ya maandalizi waliochaguliwa na Baraza la Maaskofu.

Katika ufunguzi wa Mkutano huo wa kimataifa wa vijana ulifunguliwa tarehe 5 Aprili 2017 , Kardinali Kevin Farrel Rais wa Baraza Kipapa kwa ajili ya Walei, familia na Maisha amewawakaribisha kwa niaba ya Baba Mtakatifu Francisko akisema ni mkutano wenye kuwa na umuhimu mkubwa kwa ajili ya maisha ya Kanisa, ni mkutano kwa kawaidia ambao una idadi zaidi ya washiriki 300 , kama wahudumu wa kichugaji wa vijana na zaidi ni vijana. Inahitaji hekima zaidi ya pamoja , na uzoefu mwingi wa kazi na vijana ulio kusanywa kwa miaka 30 tangu kuanzishwa kwa siku ya kimataifa ya vijana , ambayo kwa sasa imekuwa ni huduma hata ya jirani kuto kutokana na  maandalzi ya sinodi ya maaskofu ambayo inahusu vijana.
Katika siku ya kwanza  mkutano huo umetazama kwa kina juu ya Siku ya Vijana dunia iliyofanyika huko Cracovia mwaka 2016: Hii ni kazi muhimu hasa kwa vijana wa Panama ambao watakuwa na ujasiri mna pia jukumu la kufanya mandalizi ya Siku ya vijana ijayo, pia ni fursa ya kupokea matunda ya kichungaji katika tukio la nchi ya Poland na katika ulimwengu. Askofu mkuu wa Cracovia  Kardinali Stanisław(Stanslau Dziwisz) Dziwisz, amefungua sehemu za kazi akisisitiza juu mambo makuu kama vile Siku ya vijana kama uzoefu wa ukatoliki wa Kanisa ,siku ya vijana kama uzoefu wa jumuia na matumaini ya dunia mpya, siku ya vijana kama uzoefu wa Kanisa linalotoka nje , na siku ya vijana kama uzoefu wa uwajibika wa  kazi ya uinjilishaji mpya.

Hata Padre Grzegorz Suchodolski, katibu Mkuu wa kamati ya Siku ya Vijana 2016 na Padre Emil Parfiniuk, muhusika wa kitume wa vijana wa Poland, wamesisitiza katika hotuba zao umuhimu wa safari ndefu ya maandalizi na namna ya kuhusisha hawali ya yote vijana , kwa kufanya ushirikiano wa majimbo yote 44 ili kuweza  kugundua kwa upande wa Vijana wa Poland utajiri wa kiroho wa nchi yao. Aidha wamesema ni katika mkutano na watu wanaotoka katika dunia nzima wakiwa na imani katika Kristo, ambao ndiyo wamekuwa ufunguo wa mafanikio ya  Siku ya vijana duniani huko Cravovia Poland.Aidha mafanikio ya Siku ya Vijana Poland wamesema yametokana na makaribisho kupitia zaidi  katika majimbo ya Poland waliyopitia mahujaji. Aidha imeshangaza zaidi juu ya ushuhuda wa mwakilishi kutoka Iraq ,ambayo ni  mojawapo ya jumuiya ya kizamni ya kikiristo  duniani, japokuwa leo hii inakabiliwa na mateso, lakini mwakilishi kijana huyo alipendelea kwa vyovyote vile kwenda Cracovia kwa sababu amesema kitendo cha kuwa kati ya vijana wote duniani, ni mojawapo ya kujisikia bora bila kuwa na upweke au kubaguliwa. Na shuhuda nyingi zilizotolewa na wawakilishi kutoka dunia nzima kama vile Corea ya Kusini, hali halisi ya Albania, Uganda na Jamhuri ya Kidominikani, wameweza kuelezawalichokipeleka na kutenda katika nchi zao kutokana  na uzoefu wao wa safari ya maandalizi na matunda ya kushiriki katika siku ya vijana kimataifa.

Askofu msaidizi Damian Muskus wa  Cracovia , amewakilisha kazi ya mchana kwa lengo la kuonesha utendaji kiufundi wa Kazi katika maandalizi, hakusahau pia kuwakumbusha maneno ya Baba Mtakatifu Francisko alivyo waelezea watu wa  kujitolea siku ya mwisho alipokutana nao kwamba, siku imekuwa ya  pamoja na kazi nyingi, lakini hasa ni sala nyingi.Kwa maana ya kwamba pamoja na kazi nyingi inahitaji kusali sana.
Kwa namna hiyo siku ya kwanza ya mkutano wa vijana imefungwa kwa ibada ya misa Takatifu iliyo ongozwa  na Kardinali Farrel ambaye katika mahubiri amesisitiza kuwa kuitwa  wakristo haitoshi , na siyo kipande cha kujibandika kuonesha ukristo huo bali  ukristo  ni matendo  na kuonesha  ushuhuda . Vijana wataridhika na kutambua kile tunacho waonesha iwapo ujumbe wa injili utakwenda na matendo yetu. Ikumbukwe mkatano huo kunzia tarehe 5 hadi 9 Aprili unafanyika katika Chuo cha Kipapa cha Kimataifa Maria Mater Ecclesiae.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.