2017-04-06 17:15:00

Baba Mtakatifu kutoa pole kwa waathirika wa mafuriko Argentina


Baba Mtakatifu Francisko ametuma barua kwa Askofu Mkuu wa Jimbo la   Fe de la Vera Cruz, José María Arancedo ,Rais wa Baraza la maaskofu wa Argentina kuonesha uwepo wake karibu kiroho kwa ajili ya wananchi walio pata maafa ya mvua na kusababisha mafuriko.Anawatia moyo viongozi wa Kanisa na wananchi kutoa ushuhuda na mshikamano kindugu  kwa ajili ya waathirika wa mafuriko. Inasadikika ni zaidi ya watu 7,000 walio athirka katika eneo mojawapo la Comodoro Rivadavia Kusini mwa nchi hiyo na zaidi ya nyumba 2, 000 kuharibika.

Kwa njia ya barua hiyo, Baba Mtakatifu Francisko ameonesha masikitiko yake na kuonesha ukaribu kiroho kwa ajili ya maelfu ya watu walio athirika na wengi kupoteza mali zao zote walizo kuwa nazo, nyumba mali na kumbukumbu za familia, ambazo amesema ni matunda  ya sadaka na kazi ya miaka mingi.Aidha  ameomba Askofu Mkuu afikishe ujumbe wake kwa waathirika wote na kuwahakikishia sala zake, akiomba mashirika ya dini, taasisi, mapadre na maaskofu kuwa karibu na kutoa ushuhuda na mshikamano kindugu kwa ajili ya wote walio athirika.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.