2017-04-06 16:21:00

Baba Mtakatifu kuandika barua ya shukrani kwa Jimbo Kuu la Milano


Kardinali Angelo Scola Askofu Mkuu wa Milano amepokea barua ya Baba Mtakatifu inayo shukuru kwa mapokezi ya waamini wote wa jimbo wakati wa tukio la ziara yake ya kichungaji Jumapili 2 Aprili 2017. Barua imesema kuwa  wakati wa ziara yake  kichungaji katika jimbo la Milano ameishi muda mzuri na kuona umoja wa Jumuya ya jimbo, ambapo amefanya uzoefu wa makaribisho mema ya furaha na watu wa milano,kwa njia hiyo anachukua fursa kutoa shukrani ya dhati kwa  Kardinali Scola, mapadre, watawa  na watu wote wa jumuiya nzima ya Milano.
Aidha amesema anao utambuzi wa jinsi gani roho ya wote walivyo mpokea na kukutana naye, na pia kuwapongeza kwa maandalizi mema yaliyofanikisha washirki wote kutoka pande zote , akikimbuka hasa vijana , na namna walivyoweza kueleza furaha yao na uchangamfu unao ambukiza.

Halikadhalika shukrani kwa  Kardinali Scola  , wahudumu wenzake, na wote waliofanya kazi hadi kufanikisha siku hiyo ambayo kwake , kamwe haitasulika ya sala, mazungmzona sikukuu. Aidha shukrani za dhati kama Khalifa wa Mtume Petro kuona kwamba Jimbo lao linaonesha wazi hali halisi ya Kanisa na jamii na kwa upande wa kila mwamini ya kwamba vyote hivyo ni ishara ya upendo.Amewatia moyo Jimbo Kuu lote la Milano ya kuendelea katika njia hiyo , wakishuhudia kila wakati bila kuchoka kueneza furaha ya Injili kwa kila sehemu , na hata zile zenye matatizo. Na mwisho amemwomba Bwana , kwa maombezi ya Bikira Maria na watakatifu Ambrosi na Carlo Borromeo,wakati huo huo akiwaomba naye bila kuchoka kumwombea , na kumalizia na baraka ya kitume.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.