2017-04-05 17:56:00

Familia za kwanza kupokelewa Vatican kutoka Syria


Hivi karibuni , familia za kwanza zilizokuwa zimekaribishwa katika nyumba tatu za Vatican , mara baadaya kusaidiwa kupata nyenzo na kujitegemea , wameacha nyumba hizo kwa ajili ya familia nyingine mbili za akristo na familia mmoja ya kiislam kwa pamoja zikiwa na idadi ya  watu 13.
Taarifa kutoka Mfuko wa Kitume kwa ajili ya mapokezi ya wakimbizi Vatican imesema,hawa ni Familii mbili kutoka Siria wamepata matatizo ya kutekwa nyara na kubaguliwa kwaa jili ya dini yao ya kikristo na ambao wamefika nchini Italia mwezi wa 3 mwaka huu.

Familia ziliacha nafasi kwa wengine walifika nchi Italia tangu Januari 2016, kwas asa watoto wao wanakwenda shule kama kawaida na , mama wa watoto amejiandikisha katika katika kozi za masomo ya juu hasa kwa upande wa elimu ya utamaduni na maridhiano. Wakimbizi hawa wampata msaada wa kuinga nchi Italia kupitia njia halali kwa njia ya mashirika matatu yanayaojikita katika huduma hiyo kama vile Jumuiya ya Mtakatifu Egidio,makanisa ya kiinjili, na Valdesi .

Hiyo ni kutokana na kujibu ombi la Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana tarehe 6 Septemba 2015 wito ulio kuwa unahusu kuwapokea familia katika kila parrochia , Jumuiya mbalimbali watawa , madhabahau na taasisi zenye uwezo wa kufanya hivyo .Kwa njia ya mshikamano wa vyama hivyo, familia 70 zenye idadi watu 145 zimepokelewa. Pamoja na hayo Parokia Jumuiya vyama mbalimbali na  watu wakujitolea wanaendelea kuwasaidia familia kutoka Siria ili waweze kuzoea , wakiwasindikiza na kuwa karibu kuanzia katika kujifunza lugha ya kiitaliano. Pamoja na familia hizo pia ikumbukwe kwamba  kuna watu 21 waliofika na Ndege ya Baba Mtakatifu Francisko kutoka Lesbo ambao wamepata mapokezi katika maeneo ya nyumba binafsi na za watawa.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.