2017-04-05 17:35:00

Baba Mtakatifu akumbuka waathirika wa mashambulizi ya kigaidi


Mara baada ya Katekesi Baba Mtakatifu ametoa salam kwa mahujaji wote walio kuwapo na hasa pia kuwasalimia watu kutoka Poland ambao wamekuwapo Mjini Roma kufanya kumbukumbu ya miaka 12 tangu  Kifo cha Mtakatifu Yohane Paulo II tarehe 2 Aprili 2005. Baba Mtakatifu Francisko amesema yeye amekuwa shuhuda mkubwa wa Kristo mwenye bidii na mrithi wa Imani. Yeye ametoa ujumbe  mkubwa dunia kwa aina mbili yaani wa Yesu wa huruma na ule wa Fatima. Wa kwanza umekumbukwa wakati wa mwaka wa Jubileo ya huruma na wa pili unahusu ushindi wa moyo safi wa Bikira Maria dhidi ya maovu akasema,ujumbe unatukumbusha miaka mia moja ya kutokea kwa Mama Maria wa Fatima.Tuutambue na kuupokea ujumbe huo ili mioyo yetu ijazwa na kufungulia milango Kristo.

Wakati huo huo Baba Mtakatifu Francisko ametoa wito juu ya mashambulizi ya kigaidi kwenye Treni nchini Urusi ambapo shambulio hilo limesababisha waathirika wengi. Ameonesha kusikitishwa kwa janga hili na kuwaombea wote waliopoteza maisha wapumzike kwa amani halikadhalika uwepo wake kiroho kwa familia zinazo  omboleza kwa ajili ya ndugu zao.

Pia amekumbuka matukio mengine ya kutisha nchini Syria, nakusema mauaji ya kinyama katika wilaya za Idlib namna hiyo hayakubaliki , mahali ambapo wame uwawa raia kadhaa , ikiwa ni  pamoja na watoto wengi.Amesema anawaombea waathirika na kwa ajili ya familia zao. Na kutoa wito wa nguvu viongozi husika katika katika majukumu ya kisiasa na hasa katika ngazi ya kitaifa na kimataifa , ili kusitisha janga hili ,kwa ajili ya kuleta faraja kwa raia wapendwa ambao kwa muda mrefu wamechoka na vita. Aidha amewatia moyo juhudi za wale wanao jitahidi kufikisha misaada kwa wenyeji wa eneo hilo japokuwa wana ukosefu wa usalama na usumbufu.

Baba Mtakatifu Francisko pia ametoa salam kwa washiriki wa Mkutano ulio andaliwa na Baraza la Kipapa la Utamaduni , na kuwahimiza watakafakari juu ya maendeleo endelevu ya kibinadamu katika mwanga wa Sayansi ya matibabu na maadili ya kudumu. Aidha amewaalika waamini wote wa Roma kushiriki njia ya msalaba kwa ajili ya wanawake walio sulibiwa, itakayofanyika tarehe 7 Aprili 2017 huko Garbatella Roma.

Sr Anela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.