Tunajikuta katika sehemu wamapokusanyika mahujaji wengu, tuombe wote kwa maombezi
ya Mama wa Mungu, ili afungue mioyo yetu na akili zetu tuwe na neema za Mungu katika
mafundisho ya Kanisa na Neno la Mungu. Kwa njia ya Roho Mtakatifu afungue maisha yetu
na hata roho ya Kanisa ili tuutafute ukweli wa Mungu juu yetu na hata ukweli wa Mungu
juu ya binadamu.
Ni maombi ya Askofu Mkuu Henry Hoser mjumbe maalumu wa Vatican, aliyotoa kwa waamini
wote walio kusanyika pamoja katika parokia ya Mtakatifu Yakobo Medjugorje. Taarifa
kutoka Shirika la Habari la Sir linasema Askofu Mkuu wa Varsavia-Praga nchini Poland
alifika tarehe 29 Machi 2017 mchana akiwa amesindikizwa na Padre Miljenko Šteko Mkuu
wa ndugu Wafranciskani Kanda ya Erzegovina, mara baada ya kupitia nchi ya Sarajevona
Mostar.
Ikumbukwe hivi karibuni Baba Mtakatifu Francisko amemteua Kardinali Hoser Askofu Mkuu
wa Varsavia Henryk Hoser nchini Poland kwenda huko Medjugorje kwa ajili ya ziara ya
kutembelea na kuona maendeleo ya kichungaji kwa mahujaji wengi wanao fika kusali katika
eneo hilo, na hivyo ziara yake imeanza rasmi.
Alipofika Medjugorje amepokelewa na Padre Marinko Šakota, paroko wa Medjugorje
na wenzake ndugu kike na kiume wafranciskani wanao toa huduma katika parokia hiyo,
hata mahujaji. Wakati wa kutoa salam, amesema kuwa eneo hilo kwa sasa linajulikana
ulimwengu mzima. Na kuongeza kusema,Baba Mtakatifu amejali kuendeleza matendo ya toba
ya watu wanao elekea katika eneo hilo. Hii ni sehemu mojawapo ya utume na kuhakiki
utume wa kichungaji katika eneo hilo kwa kutoa mwongozo kwaa ajili ya maelekezo endelevu
ya kichungaji katika eneo hilo.
Aidha amemalizia akisema, nimekuja kutoka katika eneo lenye kuwa na ibada ya Mama
wa Mungu Maria ni Malkia wa Poland, hivyo ni matashi mema ya kwamba nanyi mpate kufanya
kama Mria Malkia katika maisha yake.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |