2017-04-01 16:08:00

Baraza la Maaskofu Afrika ya Kusini kuomboleza kifo cha H.Kathrada


Mapema wiki hii Baraza la Makanisa ya Afrika ya Kusini wakiungana na waamini na watu wote wa taifa wameomboleza kifo cha mwanasiasa mkongwe, mwanaharakati wa ubaguzi wa rangi na aliyekuwa mfungwa wa kisiasa Ahmed Mohamed Kathrada. 
Viongozi hao wa Kanisa wanamkubuka kwa kutoa salam za rambirambi kwa Bi Barbara Hogan na ukoo wote wa Kathrada kwa wakati  huu mgumu wa kuondokewa na mpendwa wao; vilevile hata  kwa chama cha Afrika ya Kusini, (ANC)na  chama cha Kikomunisti.
Ujumbe wa Viongozi wa Makanisa ya Afrika ya kusini wanasema Bwana Kathrada hakuwa Mkristo lakini aliishi maisha ya upendo kama ya kikristo mwenye kuwa na  uaminifu na uadilifu, ni mwanafunzi wa ukweli katika katika kipindi cha msimu na hata kisicho cha msimu, kujitoa, na kujitegemea kabisa bila kubakiza na hata kutoku jipendelea binafsi. Ni mfano wa wito wa binadamu na jamii yote na  wakristo wakati yeye hakuwa mkristo, na kwa maana hiyo wanaongeza, wakristo wengi wanayo ya kujifunza kutoka na mfano wa maisha yake. 

Bwana Kathrada hakuwa na  ukabila wa Afrika, lakini aliishi maadili ya Ubuntu –Botho zaidi na kushangaza wengi maana inathibitika kutoka kwa marafiki wake walio mpatia jina la ubuntubotho, siyo kuhifadhi waafrika kikabila. Kwa hakika anawakilisha maadili na kiungo muhimu katika maisha yake ya kupinga ubaguzi wa rangi Afrika ya Kusini. Hali kadhalika wamesema nchi ya Afrika ya kusini inazidi kuwa na uchungu katika muhili wa kisiasa, na hivyo wanaomba kwa matumani ya kwamba kuondoka kwa Kathy wao wasije potea, bali waweze kuwa na uamsho wa kuhamasisha maadili makuu. Kwamba Afrika ya kusini iwe na matarajio ya kuridhiana , amani , usawa na maendeleo endelevu bila kuwa na ubaguzi wa rangi, ukabila , ubaguzi wa kijisia , chuki rushwa na kunyimwa haki za chakula na malazi kwa ajili ya wote walio zaliwa na Mungu mwenye uwezo. Na mwisho wanamtakia Roho yake ipumzike kwa Amani wakati wakibaki na swali  kila asubuhi mjomba Kathy anatasema nini leo?

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.