2017-03-31 13:32:00

Maaskofu Katoliki Marekani kutoa wito wa utetezi wa mazingira


Baraza la Maaskofu wa Marekeni wakiuunga mkono Baba Mtakatifufu, wanatoa ujumbe wa nguvu katika utetezi wa mazingira kwa ajili ya kupunguza hewa ya ukaa nchini.Ni kwa mujibu wa ujumbe wa Baraza la Maaskofu kufuatia kiongozi wa Marekani Donald Trump kutoa amri ya kuondolewa kwa sheria zilizokuwa zimetiwa saini na mtangulizi wake Barack Obama kuhusu taifa hilo kuwa na nishati salama.
Ujumbe ulio tiwa sahini na Askofu Frank J.Dewane Rais wa Kamati ya Haki ya ndani na maendeleo ya binadamu ,inatoa hali ya kudhoofisha idadi kubwa ya ulinzi wa mazingira, na kuzima mipango ya kitaifa ambayo imekuwa na malengo ya  kupunguza hewa chafu katika kituo kikubwa cha umeme kwa asilimia 32% kufikia mwaka 2030.

Maagizo hayo  ya Bwana Trump, yanaweka hatari ya  malengo ya  utetezi wa mazingira, bila kuchukua hatua madhubuti kwa kuhakikisha ulinzi wa mazingira na hata viumbe wanaoishi. Vilevile maaskofu wanayo hofu ya kwamba kwa bahati mbaya maamuzi ya Trump kwa ajili ya nchi hiyo, pia yanawezekana kufikia hata ngazi ya kimataifa.Ujumbe huo wa maaskofu uliotiwa saini na  Askofu Dewane unasema sera zote  za kisiasa zinapaswa kusimamia utekelezaji wa mazingira kwa upeo wa kiujumla na binadamu, aidha wanasema kwamba baadhi ya nchi zimeweza kupiga maendeleo ya kuweza kupunguza hewa ya ukaa, na hivyo juhudi hizi hazina budi kuhimarishwa bila kuwa na vizingiti au masharti. Mwisho wa ujumbe wao wanaeleza kile ambacho anasema Baba Mtakatifu Francisko katika wosia wake wa  sifa kwa Bwana kuhusiana na ulinzi wa mazingira nyumba yetu na hivyo maaskofu wanatoa wito wa kusikiliza kilio cha nchi  na cha masikini,zaidi wale wanao ishi katika mazingira magumu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.