2017-03-30 14:24:00

Wito wenu siyo kwamba ni binafsi ni kwa manufaa ya wengine kitume!


Tumshukuru Mungu kuwapo pamoja katika kuumega  mkate wa Neno lake na Mwili wake aliotupatia.Kwa njia ya Roho Mtakatifu anatutoa katika upweke na kutugeuza tuwe kila mmoja shuhuda, ni kila mmoja lakini hata katika Makanisa yenu yote  ya Mashariki mnakotokea , kama waseminaristi, mapadri na watawa wote kike na kiume, wote mnakuwa kama mapambo ya mawe yaliyo pangwa vizuri katika Kanisa la Kristo. Uzuri wa mchumba huyo hamkupewa kwa ajili ya karama za kazi njema kwa watoto tu pamoja na kwamba wanapaswa kutenda daima na zaidi kufanya ukue , bali unapaswa uwe na usafi wa zawadi ya Mungu.Ni utangulizi wa mahubiri ya Kardinali Leonardo Sandri,Rais wa Baraza la Kipapa kwa Makanisa ya nchi za Mashariki tarehe 29 Machi 2017 wakati wa ibada Takatifu kwenye Kanisa la Mtakatifu Nicola wa Talentino kwenye Chuo cha Kipapa cha Kiarmenia Mjini Roma kwa wanachama wa Makanisa ya Mashariki.(ACCOR) Misa hiyo imefanyika wakiwa wanaadhimisha jubilei ya miaka 100 tangu kuanza kwa chama na pia  wanafunzi wakiwa wanamaliza mwaka wa masomo yao kabla ya kuondoka  kwenda katika utume.

Kardinali Sandri amesema,neema ambayo tunataka kuipokea katika kuelekea safari ya pasaka kama ilivyo utamaduni, ni kama vile hija ya chemichemi ya maji yatiririkayo kwetu sisi siku ile ya ubatizo. Na hivyo Kardinali anaendelea kusema  ni kutaka kuiishi ibada ya ekaristi takatifu katika umoja na Mapatriaki , maaskofu na waamini wote wa makanisa wanakotokea. Pia anawatakiwa matashi mema katika jubilei ya mwaka wa 100 kwani  wanaweza kufikia idhini ya mwisho wa kukubaliwa Katiba ya Chama chao ambacho kimeanza mchakato kwa muda mrefu.Akichambua juu ya somo la kwanza kutoka kitabu cha Isaya anasema, linawaalika kutafakari matendo ya Mungu kwa namna anavyotenda kwa watu wake, kwa njia yao na  kwa binadamu wote kwa maana “nilikujibu ya kwamba nilikusaidia, nilikuuumba na kukuweka, nitageuza milima kuwa barabara na kamwe sitakusahau. Kwa namna hiyo katika kipindi cha mafunzo hapa Roma , au katika huduma yoyote mnayo tenda kwenye nyumba , mnaweza kutazama matendo haya ya Mungu  kama kwamba yanawatazama ninyi.

Historia yenu ya ukombozi na ambayo ni historia yetu wote kama vile ya wafungwa, kwa maana kuna baadhi ya ndugu zetu, wa nchi za Mashariki ambao wamefungwa na wapo katika magereza ya udikteita au magaidi; Kardinali anaongeza , hata kama tumepitia katika giza  la ndani na nje ya roho , kutokana na matatizo,masumbuko au kupatwa na matukio ya nguvu na migogoro ya nchi za Mashariki , leo Mungu anasema tokeni nje, kwasababu hiyo siyo sehemu ya mwisho wa maisha. Tunapaswa kugundua wito wa imani na wito ambao ndiyo tunu msingi ya kurithi tuliyo ipokea kama zawadi.
Kardinali Sandri ametoa ushauri kwa wanafunzi wanao wanaomalizia masoma akisema;”kama watawa ambao mnajiandaa kurudi makwenu baada ya masomo,hata kwa wengine ambao baada ya masomo wamejikuta wanapewa utume mwingine, wote kwa pamoja mnapaswa kupiga hatua mbele kwa kuepuka kwamba wito mnao uishi ni wa kujiridhisha tu,yaani  kwa manufaa binafsi bila kuzaa matunda, lakini baadaye mkajikuta mna omboleza kama watu wa Sioni “Bwana amaneniacha , Bwana ameniacha”.

Tiba njema ipo  Kardinali Sandri amesema  katika kufufua kumbukumbu ya uokovu ambayo Bwana anaitenda kwenu ili pia nanyi mpate kuchangia kwa furaha kwamba yeye amekuja tena kufufua kwa upya mioyo; kama Nabii anasemavyo wazi katika agano la watu ya kwamba ni kutangaza habari njema ya uponyaji na uhuru.Hivyo muda wote mlio kaa na vitabu madarasani mkisoma isiwe kwamba ilikuwa ni kukuza akili tu kwa furaha binafsi , bali lengo kuu limekuwa ni kujikita kwa kina katika maajabu ya Mungu ambayo ninyi ni mashahidi. Kwa wale ambao mmeitwa kubaki Roma kwa shughuli za kitume na siyo kwa ajili ya masomo mnapaswa kuishi katika unyenyekevu na wepesi katika huduma mliyo kabidhiwa bila kusahau watu wa Mungu mlio chaguliwa kuwahudumia.Jambo muhimu ni utambuzi  wa Yesu anayepaswa kukaa ndani mwetu , na kwa njia hiyo kamwe tusisiite kuomba nguvu ya Roho Mtakatifu kama vile Katika Injili, Mtakatifu Yohane anatufanya tugundue siri ya uhusiano wa kina na Baba yake. Yeye hawezi kufikira lolote  nje  ya uhusiano huo.Na katika uhusiano huo ndiyo chanzo cha chemichemi inayosimamia utume wake kwa ajili ya wokovu kati ya watu.Kuwa na hisia ya kupendwa na Yesu ni sawa na kuona jinsi ambavyo afanya Baba, ndiyo anavyo tenda mwana wake, kwasababu hatma yake tunamwona katika tendo la kutoa maisha yake na kufufuka , yeye anatimiza mapenzi yake kwa yule aliye mtuma.

Kujitoa wakfu maana yake ni kuchangia njia ya Yesu Mwenyewe kati ya watu.Kuwa mwenye wakfu maana yake umechagua njia  ya Kristo mwenyewe kama asemavyo Mtakatifu Paulo “ hakuna hata mmoja  wetu anaye ishi yeye binafsi kwasababu kama tunaishi ni kwa ajili ya Bwana,na kama tukifa wote tunakufa na Bwana. Kama tunaishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana. Maana Kristo alikufa akawa hai tena, ili apate kuwa Bwana wa wazima na wafu. "kardinali Sandri amesema kuwa mwenye wakfu katika nchi za Mashariki ni kwa ajili ya Mashariki , hata katika muda wa kuishi Roma , mji wa watume wa Petro na Paulo wanatualika tuzidishe karama ya kinabii. Na mwisho anasema tukiwa katika ukaribu wa mateso ya ndugu wote, ni lazima kuwa na uahakika kwamba serikalli zote za utawala wa kigaidi na mabavu, mapema au baadye wataanguka kwasababu ni Mungu tu pekee aliye wa milele. Sisis tunao taka kuwa mitume wake , lazima kuwa vyombo vya upendo wake ambao unadumu milele.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Idhaa ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.