2017-03-30 14:54:00

Kampeni ya Kanisa la Italia kwa ajili ya wahamiaji


Baada ya kumaliza Mkutano wa Baraza la kudumu la Maaskofu nchini Italia, wametoa hati ya mwisho inayogusa mada mbalimbali ya mipango ya kibinadamu.Maaskofu wametazama kwa uangalifu juu ya changamoto mbalimbali na hasa zaidi inayohusu ajira kwa jamii ya sas na wakisisitiza kwamba bila kazi hakuna adhi ya binadamu.Katika hati ya Maaskofu pia  wakitazama  juu ya changamoto hizo wamesisitiza juu ya kutoa  kipaumbele kwanza katika Kanisa hasa kuwa karibu na watu wanao ishi katika mazingira magumu.Aidha Kikao kudumu cha Baraza la Maaskofu  Italia wamepanua mawazo zaidi licha ya kuandaa  Mkutano Mkuu ujao wa mwezi wa tano kwao  imekuwa fursa ya kujadili kwa mapana na marefu kuhusu mada nyingine zinazo husu jamii ya Italia kama vile familia, vijana, mada kuhusu mwisho wa maisha, kuwapokea watoto,ugaidi wa kuandaa ,wahamiaji na pia juu ya miaka 60 ya Umoja wa nchi za Ulaya ulio adhimishwa hivi karibuni mjini Roma na nchi 27 za Ulaya.

Katika chamoto hizo za jamii ya italia wametazama ni kwa jinsi gani Kanisa linapaswa kuwa karibu na watu wote wanao kabiliwa na majaribu na kuishi katika mazingira magumu ili kuweza kupata mwanga wa roho ya kushirikishana kwa pamoja kutokana na upeo wa sasa wa jamii na sera za kisiasa kwa ujumla. Na kutazama kwa mapana juu ya mawasiliano ya kijamii, na hasa kuhusu utashi wa makuhani katika kukabiliana na changamoto inayohusu mtazamo wa elimu na mafunzo. Kwa njia hiyo suala la mawasiliano katika mjimbo ni muhimu ili kuweza kukabiliana na mipango madhubuti kwa kulinganisha haja iliyoyopo katika maeneo ya utume kichungaji kwa mujibu wa vigezo vinavyowenda na uwekezaji na endelevu .Kwa kufanikisha lengo ma lamfunzo ya elimu ya dini  , Baraza la kudumu limetoa uamuzi wa kuandika barua kwa walimu wote wano fundisha dini katoliki , kuwatumia ujumbe wa faraja kwa ujasiri na matumaini , wakati huo huo wakitajarija kufanya baadhi ya masuala mapya katika miongozo ya Kanisa katika ufundishaji wa dini katoliki.

Wakitazama kitengo cha idhaifu wa kibinadamu, hasa katika afya kwa ujumla ya magonjwa kwasabaubu ya Mswada wa sheria iliyotolewa katika Bunge la Italia hivi karibuni inayo husu mwisho wa maisha,wamesisitizia juu ya ukaribu kwa wale wadhaifu: kwani wanasema  Kanisa inayo nafasi ya kuongoza majukumu katika ushuhuda binafsi katika matendo ya utume yaliyo wazi  kwenye  elimu na umisionari kwa kusaidia watu wanaoteseka na siyo kukubali utamaduni wa kifo kijujuu tu katika kukunusha maisha.Maisha yanapaswa kuwa na utetezi japokuwa pia kuna hali kuheshimu uamuzi binafsi wakati huo huo kuheshimu  adhi ya maisha.Kwa suala la maadhimisho ya miaka 60 ya muunganao wa nchi za Ulaya , maaskofu wamesema,nchi za Ulaya zinapaswa kuendeleza roho ya utaifa wa mababa waanzilishi ili kuepuka mawazo potofu  ambayo yanaweza kuwapeleka mbali na malengo ya umoja huo.Kwa njia hiyo nchi za Umoja wa nchi za Ulaya zinaalikwa kutazama utamaduni wa Kimeditrania yaani katika  kutoa kipaumbele zaidi kwa wahamiaji wanaojaribu kuivuka bahari.

Halikadhalika wanabainisha kuwa,Kanisa la Italia linalo jukumu la kuendelea kushika hatamu na  kuwa mstari wa mbele katika kusaidia maelfu ya watu kwa kubuni mpango ya mafunzo na maendeleo ya kijamii.Kwa namna ya pekee kuhusina na suala la wahamiaji kupitia njia za mkato baharini, wanatoa shukrani kwa Chama cha kusaidia  masikini, Mashirika katika njia za kibinadamu, ambao pia wana malengo ya kuongeza kushirikishana na maparokia,mashirika ya kitawa,Caritas na Shirika la kusaidia wahamijaji,ili wakimbizi na wahamiaji wapate kuingia kihalali nchini.Pia ili kupata kukaribisha,kuunganisha na kwa maendele endelevu kwa ajili ya wote; Baraza la Maaskofu Italia wameafikiana kujenga zaidi mahusiano na Makanisa ya Afrika ya Kaskazini na nchi nyingine kwa ujumla mahali ambapo wahamiaji wanatoka

Sr. Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.