2017-03-29 14:46:00

Injili imesaidia kufanya majuto ya Wakatoliki na Waluteri!


Huu ni mkutano ambao isingewa kuwa rahisi kufanyika kwa  miaka 50 iliyopita, kwani miaka 50 hii imeruhusu Wakatoliki na Waluteri kushinda tofauti za mila na desturi walizo kuwa nazo kwa karne nyingi kutokana na matokeo ya historia ya kutambua uwepo wa Kristo kwa kila mmoja. Ni maneno ya Askofu Mkuu wa Birmingham Bernard Longley, wakati wa mahubiri yake Jumapili 26 Machi 2017 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Giorge. Ni siku ambayo Wakatoliki na Waluteri walikusanyika pamoja kufanya kumbukumbu ya Maadhimisho ya Jubilei ya miaka 500 tangu yalipofanyika mageuzi makubwa ndani ya Kanisa na miaka 50 ya maadhimisho ya mwendelezo wa majadiliano ya kiekumene kati ya Waluteri na Wakatoliki, changamoto iliyotolewa na Mababa wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican.

Misa hiyo pia ilikuwa ni fursa ya kuwaombea waathirika wa shambulio la kigaidi la wiki iliyopita huko Westminster. Katika maombi  wameshiriki hata Askofu  Mkuu wa Kanisa la  Kiluteri wa Uingereza Martin Lind na Askofu Mkuu wa Southwark, Peter Smith. Wakatoliki na Waluteri wanashukuru Injili kwamba imewashirikisha na kuonesha majuto na huzuni  kutokana na kutenganishwa kwao na mageuzi hayo. Wameahidi kutoa ushuhuda wa Injili ya kikristo katika ulimwengu uliogawanyika na kuhumizwa.

Baada ya kupitia katika kumbukumbu ya historia ya pamoja ya Wakatoliki na Waluteri nchini Ingereza na kutazama sura muhimu zilizojengwa na maaskofu waliopita, Askofu Mkuu Longley amesema leo hii Wakatoliki na Waluteri wanayo fursa ya kushiriki kikamilifi katika kujenga upya na kusali kwa pamoja kwa ajili ya umoja wa Kikristo, kwani njia hiyo inatufanya tukaribiane na wengine. Pia amesema  hiyo ni kama kutii wito wa Kristo alio tamka yeye mwenyewe  wakati wa mahubiri yake Mlimani ya kwamba “ninyi ni chumvi ya dunia”. 

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.