2017-03-29 15:21:00

Dada wadogo wa Yesu wameancha utume baada ya miaka 60 Afghanstan


Baada ya miaka 60 ya huduma kwa wahitaji , imelazimika kuacha mji wa Kabul,hawa ni watawa wa Shirika la Dada wadogo wa Yesu.Watawa hawa wamekaa kwa muda mrefu na masikini nchini Afghanstan wakiwasaidia watu kwa kile walichoweza. Kufunga kwa nyumba zao huko imetokana na Ukosefu wa miito.Hayo yameelezwa na Padre Giuseppe Moretti ambaye amefanya utume kwa muda wa miaka 18 mji Mkuu  Kabul kama msimamizi wa Kanisa lao dogo.Padre huyo amekuwa kwa muda mrefu na hakuacha mji mkuu wakati wa maingilio ya jeshi la Kisovietiki na hata kwa wanajeshi wa kitaleban au wakati wa mabomu ya hapa na pale.

Akitoa ushuhuda juu ya historia ya watawa hawa anasema; kuwa kipigo na mateso ya namna hii yamewafanya watawa hawa kuishi na watu karibu, hata walipofika wanajeshi wa Nato mwaka 2000 kutaka kuwahoji watawa hawa hawakupendelea kutoa habari zozte kuhusu watu wao walio kuwa wakiishi nao.Hiyo siyo kwa sababu ya kuogopa ya kwamba wataonekana kama wapelelezi bali ndiyo ilikuwa mtindo na karama yao ya kuhudumia watu kwa ukimya katika mateso. Watu wengi walifika kwa watawa  kuomba msaada,waliwasikiliza kwa upendo historia zao na zilibaki ndani ya mioyo yao.Ili kuweza kushirikiana na wakazi hao,watawa hawa waliweza kuongea lugha ya wenyeji ili kushiriki bege kwa bega na watu rahisi na masikini , kwa njia hiyo watawa walipendwa na kusifiwa na jumuiya nzima ya watu kiasi kwamba miaka ya hivi karibuni  walikuwa wametunikiwa uraia wa Afghanstan.

Watawa wa Dada wadogo wa Yesu waliheshimiwa sana hata na maaskali wa Waktalebani. Anakumbuka kwamba mwaka 1993 wakati wa vita,  Ijumaa wote walikuwa wanakwenda hata katika kikanisa cha Ubalozi kusali, japokuwa Kikanisa hicho kilikuwa imefungwa kwa sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Watalebani waliwatambua ni wakina nani na hivyo waliaacha waingie kusali. Mbele ya Kikanisa hicho kuna msalaba mkubwa unao onekana Nyumba ya watawa hao ilikuwa karibu na sehemu ya ubalozi, kwa njia hiyo wangeweza hata kuharibu Kanisa hili lakini hawakufanya hivyo. Japokuwa mtawa wa mwisho kuondoka ilikuwa ni mwezi Februarari 2017,lakini historia yao ni muhimu kabisa katika nchi hii ya Afghanistan,Padre Moretti anaongeza.

Hawa ni watawa walio itikia wito kujibu upendo wa  Mungu  na kumfuasa Kristo katika kuliishi Injili ya Roho ya Betlehemu na Nazaret. Ni roho iliyo jikita katika ukimya  wa kujitoa, sala , urafiki na matendo kwa kukumbatia ulimwengu. Shirika hili lilianzishwa na Mgdaleine wa Yesu kwa ushirikiano na Mwenye heri Charles de Foucauld maarufu kama Padre wa kiroho aliyeishi katika maeneo ya jangwa. Mwenye heri Charles de F. anakumbukwa sana na wosia mwingi wa kiroho katika maisha ya waamini kila siku kwani ni kutokana na uzoefu wake kabla ya kumtambua Mungu ni nani kwake, nawakati anajitafakari maisha yake aliandika maneno kwa kumwelekea Mungu akisema “kama upo ee Mungu nipe neema ya kukutambua” lakini  baada ya kumjua ya kwamba  Mungu yupo akasema  “hasingeweza kufanya lolota zaidi ya kuwa naye mpaka milele” (1901). Kwa njia hiyo watawa wa kike na kiume wamefuata nyayo zao za Yesu wa Nazareth kwa kutoa  huduma yao pande zote za dunia.

Upendo wa Yesu Mwenye heri Charles de F. ulisababisha yeye kuwa ndugu wa wote bila ubaguzi na ameandika kwamba “utume wangu unapaswa uwe wa wema. Kwasababu atakaye niona lazima asema kwakuwa mtu huyu ni mwema na hivyo dini yake lazima ni nzuri”.Vilevile anasema  “kama nikiulizwa kwa nimi mimi ni mpole na mwema, lazima kusema kwasababu mimi ni mtumishi wa mtu aliye mzuri zaidi ya mimi”. Anaongeza , ”Kama tungelijua jinsi gani Bwana Yesu ni mwema,… ninatamani niwe mwema zaidi hadi wasema , kama mtumishi huyo ni mwema hivyo , Je Bwana wake yuko je?”.
Mwanzilishi mkuu wa Shirika Charles de Foucauld akiwa naa Mgdaleine wa Yesu ameandika tafakari nyingi sana za kiroho kuonesha upendo mkubwa wa Yesu alio kuwa nao ambazo ni urithi kwa waamini wengi , pamoja na kwamba ndiyo mwongozo wa dada wadogo wa Yesu ambao kwa miaka 60 wameweza kufanya huduma ya kitumea katika nchi ya Afghanstan na sasa wameng’atuka kwasababu ya kukosefu wa miito katika eneo hilo.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.