2017-03-26 16:28:00

Papa amesema Kanisa lisiogope changamoto maana zinalifanya likue


Unjilishaji,ushemasi na pembezoni.Ni mambo muhimu ambayo Baba Mtaaktifu Francisko ameweza kuzungumza kwenye Kanisa Kuu la Jimbo kuu la  Milano, Jumamosi tarehe 25 Machi 2017 wakati, akijibu maswali ya padre, shemasi na mtawa mmoja. Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa Kanisa halipaswi kuogopeshwa na changamoto hizo,kuona kwamba ni fursa za kuanza upya kutangaza Injili kwa watu wote.Anasematunarusha nyavu katika uinjilishaji ,tunapaswa kukumbuka kwamba siyo sisi tunao chukua samaki, bali ni Bwana  nayevua samaki hizo.Baba Mtakatifu Francisko ametumia mfano huo kuanza kujibu maswali hayo, na hasa akimjibu Padre Gabriel Gioia juu ya changamoto za jamii iliyopanuka kwa Kanisa. Anasisitiza hawali ya yote ya kwamba changamoto kwa Kanisa daima ni chachu, kwasababu hatupaswi maana zinafanya Kanisa likue.

Hiyo ni ishara ya imani hai ya jumuiya inayoishi, ambayo inamtafuta Bwana, pia kufanya macho yabaki wazi.Tunapaswa kuogopa hawali ya yote imani isiyo na changamoto, ambayo ni kujisiki kwamba umetosheka,kutokuhitaji lolote ,kila kitu kimefanyika, Hiyo siyo imani na haitajiki bali tunapaswa kuiogopa. Baba Mtakatifu Francisko ameonya juu ya baadhi ya itikadi, kwasababu anasema itikadi hizo zinatokana na mtu kujiona kwamba anayo imani iliyokamilika. Lakini Changamoto zinatuokoa kutoka katika mawazo yetu finyu na kutufungua upeo wetu kuwa mpana.
Kujuhusu kuwa na tamaduni nyingi katika jamii zetu, Baba Mtakatifu anatoa onyo kwamba hatupaswi kuogopa utofauti ,kwa utambuzi ya kwamba Kanisa ni moja,bali katika uzoefu wa aina mbalimbali na ndiyo utajiri wa Kanisa."Kanisa ni moja katika utofauti lakini ni kanisa moja". Na utofauti huo unaunganishwa kuwa katika umoja. Lakini je ni nani anayefanya tafauti? Ni roho Mtakatifu , ambaye ni mwalimu wa utofauti.Ni nani anayefanya umoja? Ni Roho Mtakatifu Mwenyewe,akiwa mwalimu wa umoja. Ndiye msanii mkubwa, ndiye Mwalimu wa Umoja na katika utofauti ni Roho Mtakatifu.Anasisitiza kwamba hilo tunapaswa kulitambua vema.

Aidha Baba Mtakatifu Francisko anatoa mfano kwamba ulinganifu na wingi zaidi haviendani na siyo mambo yatokanayo na Roho Mtakatifu, bali wengi zaidi na umoja vinatokana na Roho Mtakatifu na kwa njia hiyo anasisitiza juu ya kufanya  uamuzi. Kwa kuwasaidia vijana waweza kuamua yaliyo mema katoka katika utamaduni ulio saza. Kwa mfano  anasema vijana wetu wako tayari kuchat kila wakati .Wanauwezo kuchat kwa kutumia aina mbili ua tatu za skrin kwa wakati mmoja, na wanawaza kuingiliana kwa wakati mmoja katika matukio mbambali yanayoendelea.Hivyo anasema tupende tusipende ndiyo namna walivyo jikita ndani yake, na kwa njia hiyo sisi kama wachungaji tunao wajibu wa kuwasaidia katika ulimwengu huu.Anaongeza,"nadhani ni vizuri kuwafundisha kupembua ,kwasababu tunazo zana na vifaa vya kuweza kuwasaidia kutembea njia ya maisha bila kuzima Roho Mtakatifu aliye ndani yao".

Shemasi awe mlinzi wa huduma ya Kanisa.Baba Mtakatifu amemjibu Shemasi Roberto Crespi ambaye ni shemasi wa kudumu na kwa namna ya pekee katika huduma yake ya ushemasi.Ameonesha mara moja kuelezea juu ya umuhimu  na mchango mkubwa wa maisha ya Kanisa.Lakini pamoja na hayo ametoa onyo mara moja juu ya  hatari mbili za huduma ya shemasi, ya kwanza ile ya kiulimwengu na pili ya kufanya kazi zaidi. Baba Mtakatifu anasema Shemasi ni mlinzi wa huduma ya Kanisa. Akichambua maana ya huduma anasema ni ufunguo unaolezea jukumu ya huduma yao, wito wao na wao wenyewe kuwa Kanisa.Wito ndani ya wito kama miito mingine na siyo ya kibinafsi, bali inapaswa kuishi ndani ya familia na familia. Ndiyo ya watu na watu wa Mungu. Maana yake ni kwamaba hakuna huduma altare na hakuna liturujia ambayo aijifungui katika huduma ya masikini , na hakuna huduma ya masikini ambayo haifungujki katika liturujia.Hakuna jamii ya kazi  ambayo siyo ya kifamilia.Hiyo inatusaidia kupembua ushamasi kama wito wa Kanisa.Amesisitiza Baba Mtakatifu.

Akijibu swali la mtawa Paola Paganono juu ya changamoto za kikrsto ya kuwa ni  wachache ndani ya jamii ya sasa. Baba Mtakatifu amesema kitendo cha uchache kisiwe kisingizio cha kutokuwajibika ,kwani tukumbuke daima kwamba ni kiasi kidogo cha chachu kinachohitaji kufanya unga ukue. Ni bora kuanza mchakato badala ya kujaza nafasi.Leo hii tunapaswa kuanza michakato badala ya kujaza nasasi , kupambana kwa ajili ya umoja badala ya kusimamia migongano iliyopita, kusikiliza hali halisi,kujifunua katika wengi kwa watu wa Mungu na wote wa Kanisa,maana yake kujifungua kikanisa. 
Baba Mtakatifu pia amezungumzia juu ya ushuhuda wa watawa wawili Shrika la watawa  wa dada wa Yesu huko Afghanstan, na kusema inabidi kwenda katika maeneo ya pembezoni na kuwa wamisionari, kwenda kukutana na watu , kukutana na Bwana katika miisho ya dunia.Na hiyo ndiyo manaa ya kwenda.Kuchangua sehemu za pembezoni,na hivyo amesema  "amkeni na kuanza mchakato, washeni matumani mahali ambapo yamezimika, katika jamii iliyogeuka na kutokuona uchungu wa wengine. Katika udhaifu wetu, kama vile shirika linaweza kuwa makini kwa wote  walio dhaifu, na baadaye wakageuka sehemu yenye kuwa na baraka".

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.