2017-03-25 17:11:00

Tukubali hata sisi kama Kanisa ukarabati kwasababu tu wadhambi!


Jumamosi tarehe 25 Machi 2017 ,Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Milano katika ziara yak e ya kitume, alikwenda moja kwa moja eneo la pembezoni mwa mji kuwatembelea na kuwaona wakazi wa hapo Forlanini nyumba nyeupe. 
Amewasalimia na kuwakuwashukuru kwa makaribisho yao kwasababu ya kumpokea katika mji wa Milano na kuingi katika nyuso za familia na jumuiya hiyo.Anawashuru pia kwa zawadi mbili walizo mpatia , moja ikiwa ni stola na kusema ni ishara ya ukuhani, inanigusa kwa namna ya pekee kwasasababu ya kukumbuka ya kwamba nimekuja kati yenu kama kuhani, nimekuja Milan kama Padre.Na  hiyo stola siyo kwamba mmeinunua bali imetengenezwa hapa kwa kazi ya mikono ya baadhi yenu.Kwa njia hiyo inatoa thamani kubwa; na kukumbusha kwamba kila kuhani mkristo amechaguliwa na watu kwa ajili ya huduma ya watu, ukuhani wangu, ni kama vile ukuhani wa Paroko wenu na wengine wanaofanya huduma hapa ni zawadi ya Kristo, lakini pia ni kitambaa chenu cha watu wetu, kwa imani yao katika ugumu wa kazi yenu, sala zenu, na machozi yenu, vyote hivyo naviona katika ishara ya stola hii amesema Baba Mtakatifu.

Aidha amesema mmenizawadia picha ya Mama Maria wenu :kama ilivyokuwa tangu mwanzo na hata baada ya kukarabaitiwa.Ninatambua ya kwamba Mama Maria ananipokea Milan katika Kinara cha Kanisa Kuu: Lakini ninawashukuru kwa zawadi hii kwasababu tayari mama Maria amenipokea kuanzia hapa na hiyo ni muhimu. Inanikumbusha ukarimu wa Mama Maria aliyekimbia kwenda kukutana na Elizabeth.
Ni ukarimu na motisha kwa Kanisa ambao haupaswi kubaki unasubiri, bali kuondoka na kwenda kukutana na wote, katika sehemu za pembezoni, Kanisa linakwenda kukutana hata wasio wakristo,na hata wasio aminiili kuwapelekea Yesu ambaye ni upendo wa Mungu aliye fanyika mwili, na yeye analeta maana ya maisha yetu na kutuepusha mabaya.Kuna maana kubwa ya ukarabati wa sanamu hiyo, kwasababu ukarabati wa sanamu ya mama Maria ni ishara inajioeleza kwa Kanisa  kwamba daima linahitaji kukarabatiwa kwasababu Kanisa limetengenezwa na sisi tulio wadhambi.

Tukubali kukarabatiwa na Mungu kwa huruma yake. Tukubali kusafishika mioyo na hasa katika kipindi hiki cha kwaresima. Mama  Maria mwenyewe hana dhambi na hana haja ya kukarabatiwa, lakini sanamu yake ndiyo, hivyo kama mama anavyo tufundisha, tukubali kusafishwa na huruma ya Mungu ili tuweze kuwa mashuhuda wa utakatifu wa Yesu.Ninawashurku kwa moyo wote kwa zawadi hizi, na zaidi asante kwa uwepo wenu, kwa ajili ya makaribisho yen una sala zenu za kunisindikiza kuingia Milano, Mungu awabariki na Mama Maria awalinde.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.