2017-03-25 12:01:00

Askofu mkuu mteule Guzman ateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Chad


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu mteule Santiago DE WIT GUZMÁN kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Chad na ataendelea kuwa pia Balozi wa Vatican huko Jamhuri ya Watu wa Afrika ya kati. Askofu mkuu mteule Santiago De Wit Guzman alizaliwa tarehe 5 Septemba 1964 huko Valencia, nchini Hispania. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi kunako tarehe 27 Mei 1989 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Askofu mkuu mteule Santiago DE WIT GUZMÁN Alianza huduma ya kidiplomasia mjini Vatican kunako tarehe 13 Juni 1998. Tangu wakati huo, ametoa huduma yake huko Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati, Netherland, Paraguay, Misri, DRC na Hispania.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.