2017-03-24 16:00:00

Wenyeheri Francesco na Yacinta Marto kutangazwa watakatifu!


Baba Mtakatifu Francisko tarehe 23 Machi 2017 amekutana na Kardinali Angelo Amato Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya machakato wa kuwatangaza watakatifu.Baba Mkatifu amepokeana kutoa ruhusa ya Baraza hilo kuwatangaza mwenyeheri Angelo da Acri Padri wa Shirika la ndugu wadogo Wakapuchini aliyezaliwa Oktoba 1669 na kifo chake 30 Oktoba 1739. Mwenye heri  Francesco Marto, aliyezaliwa 11 Juni 1908 na kifo chake kikatokea hapo 4 Aprili 1919 na Mwenyeheri Yacinta Marto, aliyezaliwa 11 Machi 1910 na kifo chake  20 Februari  1920, hawa watoto ni ndugu wawili wa Fatima.

Watumishi wa Mungu Giuseppe Maria Fernández Sánchez na wenzake  32 mapadiri wa Shiriki la kimisionari, na pia walei 6 wa chama cha medali ya miujiza ya Bikira Maria, walio uwawa mwaka 1936 kwenye vita  nchini Hispania.Mtumishi wa Mungu  Regina Maria Vattalil mtawa wa Shirika la watawa wa ndani wa Mtakatifu Clara. Mtumishi wa Mungu Daniel Padre Mkapuchini aliyezaliwa  15 Juni  1876 na kifo chake tarehe 19 Mei 1924;Mtumishi wa Mungu Macrina Raparelli Mwanzilishi wa Shirika la watawa wa kike Basiliane wa wana wa makrina aliyezaliwa 2 Aprili 1893 na kifo chake tarehe 26 Februari1970. Mtumishi wa Mungu Daniela Zanetta, Mlei aliyezaliwa 15 Desemba  1962 kifo chake 14 April 1986.

Vilevile Baba Mtakatifu Francisko ameridhia maombi kutoka katika ngazi ya Makardinali na Maaskofu wa Baraza hilo kuwatangaza watakatifu, mwenye heri Andrea de Soveral na Ambrogio Francesco Ferro,mapadre wa Jimbo na Matteo Moreira, mlei na wanzake 27 mashahidi walio uwawa kwa ajili ya kutetea imani yao nchini Brazil tarehe 16 Julai 1645 na tarehe 3 Oktoba 1645. Na mwisho Cristoforo, Antonio na  Giovanni, vijana mashahidi walio uwawa kwa ajili ya kutetea imani yao nchini Mexco mwaka 1529. 

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.