2017-03-23 14:24:00

Papa Francisko asikitishwa na shambulizi la kigaidi London!


Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa sana na shambulizi la kigaidi lililotokea Jijini London, Jumatano, tarehe 22 Machi 2017 na kusababisha watu kadhaa kupoteza maisha na wengine wengi kupata majeraha. Baba Mtakatifu katika salam za rambi rambi zilizoandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwenda kwa Kardinali Vincent Nichols, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Uingereza na Wales anasema kwamba, anapenda kuonesha uwepo wake na mshikamano wa dhati na wale wote walioguswa na maafa haya.

Baba Mtakatifu anawaombea wale waliofariki dunia, huruma ya Mwenyezi Mungu pamoja na kuwaombea nguvu na amani ndugu, jamaa na marafiki wote. Baba Mtakatifu Francisko anapenda kuwahakikishia wananchi wote wa Uingereza uwepo wake kwa njia ya sala katika kipindi hiki kigumu!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.