2017-03-21 16:45:00

Wasiwasi wa Baraza la Maaskofu Italia juu ya changamoto za jamii


Uzuri na mahitaji ya familia, umejengwa juu ya ndoa maisha ya ndoa yaliyo wazi, hayatashindwa kamwe ingawa kwa namna ya pekee kuna baadhi ya taasisi za familia kuendelea kukuza aina nyingine ya muungano ambao ni tofauti, na maadnili ya hali halisi ya ndoa. Ni maneno ya utangulizi wa hotuba ya Kardinali Angelo Bagnasco Askofu Mkuu wa Genoa na Rais wa Baraza la maaskofu wa Italia.Kardinali Bagnasco anarudi katika mada ya familia kwa kupinga dhana za mawazo potofu ya kuunda familia, ambayo yametokana na matunda ya itikadi  za kisasa yaani upeo wa kiitikadi zinazokwenda kinyume na maadili. Katika uchambuzi wa kawaida wa hali halisi ya kijamii nchini Italia ,Rais wa Baraza la maaskofu anabainisha shehemu mbalimbali kama vile familia, vijana , katika kazi na misingi ya dharura kubwa ambavyo vinahitaji tahadhari na kusimamiwa kikamilifu na taasisi husika.
Anasema hawakati  tamaa kutoa wito katika sera za kisiasa ili ziweze kutambua yaani kuwa na upendo kwa kutoa huduma kwa watu,kuwa makini katika kushughulikia masuala kama vile kazi, familia ,vijana  na pia idadi ya watu wanao angaika kipindi cha baridi.

 Anasisitiza; kuna haja ya  uhalisia wa kisiasa, na amani kitaasisi kujikita katika kushughulika masuala haya.Halikadhalika pamoja na uwepo wa baadhi ya ishara nyanya , Kardinali Bagnasco anatoa mfano wa kipeo cha haraka kinachopaswa kutazamwa kwa uangalifu na hasa juu ya ajira kwa vijana, na kusema mikoa inayopaswa kutazamwa kwa ungalifu ni mikoa ya kusini mwa Italia, kwani imefikia asilimia 57%, wakati wastani wa kitaifa ni asilimia 40%. Pamoja na masuala kuhusu ajira , bado kuna wasiwasi mkubwa unaozidi  kushuka yaani idadi ya watu. Kwa mwaka 2015 watoto walio zaliwa walikuwa 480,000 na katika mwaka 2016 ni mwaka ulio tia rekodi mpya kuzidi kushuka chini ya 474,000 tu( ambayo ni asilimia -2,4%)
Akitazama kwa upande wa watoto na elimu, Kardinali Bagnanaso anasema ,mkwa mtazamo juu ya watoto hasa katika ngazi  ya utume kichungaji kwa miaka sasa imaeanza kuwa changamoto ya elimu, ambapo anasema hawawezi kuacha kurudia kutoa wito upya kwa taasisi zote , wazazi na taasisi mbalimbali.Akikumbusha juu ya wito wa Baba Mtakatifu Francisko kuhusu wasiwasi mkubwa juu ya suala la jinsia.

Katika wosia wa “sifa kwa Mungu, anaonesha wasiwasi huo anaposema kwamba;kuna  baadhi ya nchi za Ulaya , ambazo wameanza kuhamasisha tamaduni ya jinsia. Yapo mazingira ya mtu kwasababu mtu anayo asili yake ambayo ni lazima kuheshimiwa na kwamba haiwezekani kuiendesha namna kiholela,(Sifa kwa  Kwangu 155).Aidha katika moja ya hotuba zake anasema tunayo hatari kubwa ya kurudi nyuma kkama kuna mawazo ya kuondoa utofauti. Kwa njia hiyo Kardinali Bagnasco anawataka watu wazima kuwa macho katika itikadi hizi za sasa kwa ajili ya watoto.Kardinali anatoa swali, je kuna sera ambazo wanatia moyo kusaidia kiwango cha uzazi watoto?; Ana orodhesha baadhi ya matatizo yanayo sababisha kupungua kwa watoto nchini Italia ikiwa pamoja na ukosefu wa ajira , kodi zaidi za binadamu na pia baadhi kuanzishwa majukwa ya familia yenye mtazamo tofauti ya mpango wa uzazi.Pamoja na hayo bado anaelezea matatizo mengine juu ya sheria ya mwisho wa maisha, ambayo kwa sasa iko katika mchakato bungeni.

Kwa upande wake binafsi, anasema inabidi kutetea maisha hadi mwisho , kwani mgonjwa anapaswa asindikizwa kwa uangalifu, daima apate upendo mkubwa, maana maisha ni matakatifu.Katika hotuba yake, pia hapakosekana suala la uhamiaji ,pamoja na hayo anawapongeza kwa shughuli na mshikamano ulio oneshwa na wakazi wote wa Italia kujaribu kutafuta kwa pamoja ushirikiano katika ngazi ya kimataifa, pamoja na kushirikiana kwa matendo ya Kanisa katika nchi ya italia.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.