Shirika la Kipapa la kuhudumia Makanisa hitaji wameandaa makutano kuanzia tarehe
23 hadi 27 Machi 2017 katika miji mitatu ya Ufaransa na Monaco,makutano hayo yanaitwa
“Usiku wa Mashuhuda”.
Katika makutano hayo watatoa ushuhuda Padre Jacques Mourad kutoka nchi ya Syiria
wa Jumuiya ya Mar Moussa ambaye kwa miezi mitano alikuwa ametekwa nyara na inayojiita
serikali ya kiislam, Padre Philippe Blot mmisonari mmoja wa Paris, anayejishughulisha
na wakimbizi kutoka Korea ya Kaskazini, Mtawa Marie-Catherine Kingbo Mwanzilishi
wa Shirika watawa wanawake la Watumishi wa Kristo huko Niger.Hawa watakuwa mashahidi
wakuu watatu katika usiku shuhuda kwa mwaka 2017.
Pamoja na shuhuda hizo kwa namna ya pekee katika Kanisa kuu ya Notre Dama kwenye
Mji Mkuu Paris ,Ijumaa 24 Mchana misa Takatifu itaadhimisha na Askofu msaidizi Jérôme
Beau .Baada ya maadhimisho itafuata mkesha. Makutano ya ushuhuda huo umefikia mara
ya 9 tangu yaanzishwe, kwa lengo kutaka watu watambue hali ngumu na manyanyaso yanayo
endelea kuwakumba wakristo, katika kutafuta namna ya kuzuia na pia kurokuendela kunyamaza
kuhusiana na matukio hayo.Taarifa zinasema watu watatu walio alikwa kutoa ushuhuda,
wataongela zaidi juu ya shughuli zao za utume.
Pamoja na hayo watafanya maandamano ya sala wakiwa na picha za mapadre na watawa ,
walio uwawa miaka ya hivi karibuni kutoka nchi ya Mexco, Jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo na nchi nyinginezo duniani kote.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |