2017-03-17 14:20:00

Tuwe na mazoea ya kusali Malaika Mlinzi maana ni msindikizaji


Mimi ninafikiria daima  kwamba  Mungu yupo, hayo ni maneno ya mwigizaji mmoja kutoka Italia Valeria Fabrizi kwenye mfululizo wa Filamu katika televisheni yenye kichwa cha habari ”Ili Mungu atusaidie” .Anasimulia historia binafsi ya kiroho katika mwendelezo wa mazungumzo na Mungu ya kwamba ni  Yeye anayetuongoza, ameisha andika yote yanayotokea kila siku katika maisha yetu na  hiyo ndiyo zawadi isiyo kifani  ambapo tunapaswa kumshukuru kwa yote madogo na makubwa ya furaha anazotujalia kila siku, hiyo diyo sala kwa upande wake!
Kwa upande wa Filamu “ili Mungu atusaidie” imekuwa maarufu sana nchini Italia na kuwa na watazamaji wengi, kutokana na kwamba matukio ya picha hiyo ni matukio ya jamii ya sasa,pamoja na kwamba filamu hiyo inajionesha katika mazingira ya kitawa.Inaonesha jinsi gani watawa wako katika heke heka za shughuliza zao kila siku kuwapokea na kuishi na watoto wenye shida, vijana, familia mbalimbali, wanawasindikiza mashuleni, mahakamani, hospitalini,na zaidi pia kujihussha na utetezi wa haki ya watoto, wanawake, ambapo wako tayari kufanya kazi na wawakili, hata kufanya upelelezi ili kusaidia kutafuta sukuhisho la kijamii ambalo ni changamoto za jamii mahalia Italia lakini katika ulimwengu.

Tukirudi katika ushuhuda, kwa njia hiyo Valeria Fabrizi lakini jina la mtawa analotumia katika filam ni Costanza,  mahojiano anaendelea kueleza kwanini kusema asante kwa Mungu?; Ni kwasababu, yapo  mambo mengi ya kumshukuru mungu kwa upendo wa kweli na  kumshukuru kama mtoto.Upendo ni wajibu wa kila mtu lakini pia  katika maisha yote ya binadamu, ambapo inabidi kuwa na utambuzi wa Baba mama na mwana  kwa maana nyingnie tunaweza kusema ni kama utatu.Aidha  anatoa ushuhuda wa maisha yake kuwa daima amekuwa muumini kwa mambo matakatifu,kwa mfano,alipokuwa mdogo alizawadiwa picha ndogo ambayo aliitunza na ikaweza kumsindikiza kila mahali alipokuwa akitembea.Baada ya kuanza  kazi katika kiwanda kimoja, pia alizawadiwa picha nyingine lakini pia ilikuwa inafanana ya kwanza yaani ikionesha uso wa Yesu.Na kwa mara nyingine tena Paroko wa Parokia yake alimzawadia  picha nyingine nayo ilikuwa ni picha ile ile ya Yesu. Ndipo siku moja paroko akampeleka kutembelea Kanisa moja karibu na Vatican, kwasababu yeye hakuwa mkazi wa Roma, kuingia katika Kanisa hilo alikutana na asili ya Picha  aliyokuwa amezawadiwa tangu utoto  wake, na kumbe ilikuwa picha ya Yesu wa Huruma.yaani picha ya Yesu.

Kutokana na kuishi kwa sasa Roma anasema mara kwa mara  anapata nafasi  ya kwenda katika Kanisa hilo, na kuchukua picha hizo ndogo kwa kuwasambazia hata wengine.Anaongeza, siyo tu picha ndogo za uso waYesu wa huruma ,bali kupitia maduka mbalimbali ya Vatican kununua rosari ndogo za Yesu wa huruma kwa ajili ya kutoa zawadi kwa wengine.Halikadhalika anasema kwamba, watu wengi hawana mazoea ya kusali sala ya malaika walinzi, lakini anaamini kwamba Malaika walinzi wapo na wanatusindikiza katika maisha yetu kila siku.
Kuhusiana na suala la nafasi yake kama mwigizaji, Valeria anatoa pia  ushuhuda namna anavyojisikia kwenye filamu katika nafasi ya Mtawa Costanza akiwa mama mkuu wa nyumba ya watawa.Katika nafasi hiyo anaeleza kuwa anaonekana kuwa yeye anayo matatizo ya afya  ambapo analazimika kumeza dawa kila siku.Kwa namna  fulani nafasi yake katika filamu inapendwa sana na watu wengi wanao tazama filamu hiyo.

Kuhusu maisha yake akiwa mdogo hakuwa anaonesha uchamgamfu japokuwa alikuwa ni mzuri, anaongeza ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kupewa vipawa vingi kama vile kuimba ,kucheza, kuigiza , katika kila sehemu ya maigizo yawe makubwa au madogo.Anaomba radhi kwamba hataki kuonesha majivuno lakini ki ukweli katika maisha yake hakutawaliwa na tamaa wala majivuno japokuwa amekuwa na mali,alikuwa akiridhika na kila jambo. 
Kadhalika katika maisha yake,alipendelea kuolewa na kupata familia ya mtoto mmoja kwani mtoto mwingine alifariki , jambo ambalo lilimfanya kuacha kazi kwa kipindi cha muda mrefu. Baada ya mme wake kufariki, mtoto wake wa kike alimshauri kutafuta kazi tena na kuanza kazi ya maigizo, hadi leo anafurahi kazi hiyo ambayo anadhani ni asili yake.Na kwanini anasema ni asili yake? kwasababu tangu akiwa mtoto alijitambua kuwa muigizaji  kwani alikuwa akifanya matukio ya kulia mara kwa mara mbele ya kioo, jambo ambalo  bibi yake alikuwa akiogopa , lakini jibu alimpatia kuwa anaigiza; kwa namna hiyo ni wazi hadi leo ndiyo kazi anayoifanya.

Katika filamu kwenye nafasi ya mama mkuu wa nyumba ya watawa , anaonesha kuwa na tabia kuu, ya utukutu wa ajabu kwa wengine , anataka kujua kila  kitu kinachotoke kwa wengine na hata  anao kutana nao, anasema , hiyo ndiyo ilikuwa tabia yake tangu mdogo. Kwa bahati nzuri anayo hekima ambapo kila mmoja anaweza kwenda kwake kuomba ushauri uwe  mkubwa au mdogo .Jambo jingine muhimu ni kuhusu kujitoa sadaka; anasema ukiwa unafanya kazi unaweza kuwasidia wengi, na kama hufanyi kazi siyo rahisi kutenda jambo la dhati , hiyo akimaanisha uwezo kifedha.Anaongeza kwamba, watu wengi wanao fanya kazi katika televisheni wanazo fedha , wanayo maisha mazuri, ni waigizaji wazuri, lakini kwa upande wa kujitoa  sadaka siyo wote wako tayari, kwasababu walio wengi wanapenda kuitwa  katika tamasha fulani  la kihisani na kuhamasisha,wakati huo wanapoitwa lazima walipwe kiasi kidogo , kwa bahati mbaya waigizaji wengine ni matajiri wa ajabu, na hawajuhi fedha waziweke wapi. Anaongeza, anasikitika kuyasema hayo lakini ni vema kusema ukweli, ya kwamba ni aibu.Anamalizia ushuhuda mwigizaji Valeria Fabrizi katika filamu “ili Mungu tusaidie “ kwenye nafasi ya mtawa Costanza!

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.