2017-03-15 14:46:00

Utafiti juu ya sababu za Vijana Marekani kuwa mbali na Kanisa


Namna ya kuwapata vijana wakubwa ambao waliondoka au ndiyo wanaacha Kanisa , ni changamoto ambayo maparokia nchini Marekani leo hii wanajikita kwa ajili ya kuanza kwa upya mara baada Baraza la maaskofu kualikwa kujibu maswali juu ya vijana wakubwa kwa ajili ya maandalizi ya  Sinodi itakayofanyika 2018 inayohusu  vijana , imani na  maang’amuzi  ya miito.Msemaji Katoliki kitaifa anasema hayo katika makala ya Nicole Sotelo ya hivi karibuni tarehe 2 Machi 2017 ,akiwaalika siyo tu maaskofu  kuwa makini kwa ajili ya vijana ambao tayari wanajishughulisha  zaidi katika maisha ya Kanisa , bali kwa namna ya pekee wale waliokwenda  mbali na Kanisa. 
Habari zinazsema ,nchini Marekani Kituo cha utafiti Pew ambao wamefanya utafiti wa kina , wameonesha wazi takwimu za watu wanao karibia kanisa na wale walio  mbali na Kanisa na kutaka kujua sababu zilizo wafanya waondoke. Takwimu hizo zinaonesha wazi kati ya wakatoliki wa Marekani wanao onekana kuwa nje ya Kanisa  ni asilimia 80%.na  ambao wamefanya uchaguzi huo kabla ya kufikia miaka 24. Na pamoja na hayo  Wakatoliki walio acha Kanisa, wameulizwa swali kwanini ya  kufanya uchaguzi huo. Kati ya maelezo waliyotoa ni yale yanayohusu mafundishio ya Kanisa na hasa kuhusiana na swala la ngono.

Asilimia 56% hawakubaliani na mawazo na maelekezo kuhusu  utoaji wa mimba,na ushoga,wakati huo huo asilimia 48% waliohojiwa wanasema hawakubali juu ya mafundisho na namna ya udhibiti wa uzazi. Utafiti ulio fanywa na kituo cha Pew  nchini Marekani pia unaonesha kuwa vijana wengi wamekwenda mbali na Kanisa kwasababu ya mtazamo wa Kanisa dhidi ya wanawake.Msemaji Katoliki Kitaifa nchini Marekani anasema, hata kati ya wakatoliki wanaoudhulia Kanisani wameonesha kiasi kikubwa ule utashi wa wanawake kutaka kuheshimiwa na kuthaminiwa zaidi utu wao na  hata katika nafsi za wajibu wao.Kwa mtazamo wa wakatoliki wasio kwenda Kanisani Marekani, ni asilimia tu 8% inayokazia macho dhidi ya Kanisa kuachilia mbali na riturjia za jadi kwa mfano wa ibada ya misa ya Kilatini.Anasema Nicole Sotelo kuwa unaweza kufikiria kwamba wale walio acha Kanisa siyo waamini wa kweli. Lakini ni kinyume kwasababu walipo kuwa watoto na vijana walikuwa wamojawapo wa Kanisa japokuwa baadaye wameweza kuondoka Kanisa kutoka kwa wale wanaofanya sehemu ya Kanisa.

Ikumbukwe utafiti huo umetokana mara baada ya mama Kanisa kuanza maandalizi ya maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya Vijana , ikiwa na Kauli mbiu Imani na Maang’muzi ya miito , itakayofanyika 2018. Kwa njia hiyo ili Kanisa liweze kupata miito mitakatifu , haina budi kusali , kuwasikiliza vijana kwa uangalifu pamoja na kutembea nao kwa matumaini. Baba Mtakatifu mara kwa mara anatoa wito kwa viongozi wote wa Kanisa, kuwa karibu na vijana ,kuwasindikiza, kuwasilikiliza mahitaji yao,wasiwe pweke .Mojawapo ya Hotuba yake kwa wajumbe wa kongamano la miito mitakatifu kutoka Majimbo mbali mbali nchini Italia mwaka jana Baba Mtakatifu Francisko  anasema vijana washirikishwe kazi za kimissionari na matendo ya huruma kwa wagonjwa, maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii. Vijana wanapaswa kuwa kweli ni mashuhuda na “majembe” ya huruma ya Mungu katika matendo ya huruma kama vile kiroho na kimwili Vijana wasipopendwa na kuthaminiwa, hawa watachoka na kuwa wachovu hata kabla ya muda wa kwenda pensheni.

Halikadhalika anasema ushuhuda wenye mvuto na uzoefu  kutoka kwa Mapadre na Watawa ni chachu muhimu sana ya miito ndani ya Kanisa. Vijana wanataka kuona Wakleri na Watawa wanao jitoa sadaka kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Kanisa; wawe ni watu wasiojitafuta wenyewe katika ubinafsi wao, kwa njia hiyo ni kusema  matendo yanazungumza zaidi kuliko maneno matupu.  Na ndiyo maana Makanisa yote katoliki Ulimwenguni yamewaalikwa kufanya maandalizi  kila sehemu kwa ajili ya ufanisi wa Sinodi ijayo ya maaskofu 2018 kuhusu Vijana.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.