Waseminari 25 wameokolewa na Kikosi cha wanajeshi wa Kulinda amani cha Umoja wa
Mataifa nchi ya jamhuri ya Kideomkrasi aya Congo (DRC). Waseminari hao waliokolewa
kutoka Mbuji-Mayi kwa njia ya helikopta , walikuwa moja ya kikundi kilichopotelea
msituni baada ya mashambulizi ya seminari yao Kuu ya Malole huko Kananga Kasai ya
Kati.Wanamgambo ni wafuasi wa Kiongozi marehemu Kamwina Nsaputarehe 18 Februari 2017.
Waseminari hao wamekombolewa baada ya wito uliotolewa na Askofu Emmanuel Bernard
Kasanda Mulenga ,askofu wa Jimbo la Mbuji-Mayi. Waseminari 25 wamerudi sasa katika
familia zao baada ya kuzuiwa kukaa Kananga kwasababu ya barabara inayo unganisha
Mbuji -Mayi kuzuiwa, kutokana na uwepo wa wanamgambo wa Kamwina Nsapu.
Ikumbukwe kwamba, tarehe 18 Februari 2017 wanamgambo wafuasi wa Kamwina Nsapu walivamia Seminari kuu ya Malole Kananga ya Kasai ya Kati katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo . Wanamgambo hao walivunja mitambo ya kulinda seminari hiyo,walivunja milango yote na kuwaingilia. Waliharibu vyumba vyao na kila kitu kilichokuwa ndani, pia kuingilia vyumba vya walimu wao na kuchoma masanduku yao.Taarifa hizo zilitolewa kwa njia ya Radio Okapi na Gombera wa Seminari hiyo Kuu Padre Richard Kitenge . Hata tarehe 18 Februari 2017 Baba Mtakatifu Francisko aliwakumbuka watu hao wakati wa sala ya Malaika wa Bwana na kutoa masikitiko yake juu ya uharibifu na nguvu wanao fanya wanamgambo hao wa kiongozi Kamwina Nsapu aliyeuwawa mwezi Agosti mwaka jana.Naye Askofu Félicien Mwanama Galumbulula alikuwa amelaani vitendo vya kutisha visivyoelezeka dhidi ya watu kutokana na wanamgambo hao.
Sr Angela Rwezaula
idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |