Kuunganisha ngoma, muziki katika tamasha ndiyo dhamira kubwa ya kuwafanya vijana
wagundue furaha ya Injili.Ni lengo la baadhi ya ndugu wadogo wa Shirika la Mtakatifu
Francisko wa Asisi ambao kwa miaka mingi wamejihusisha katika utume wa uinjilishaji,na
kujituma kuweka uhai kwa kuandaa tamasha lenye kauli mbiu “wewe ni mzuri na ndiyo
maana uko duniani”.
Hii ni sala katika muziki ,ni kipindi cha kufungua moyo wa matumaini na imani kwa
Mungu,ni wakati wa kujisikia kitu kimoja, ni kukaa pamoja katika njia hiyo na kushukuru
Mungu kwa maisha uliyopewa:”Wewe ni mzuri kwa maana hiyo uko duniani”.Tamasha la
uinjilishaji lilifikiriwa na kuanzishwa na ndugu wadogo wa wafranciskan, licha ya
kwamba mawazo yao hayo pia yamekubaliwa na waimbaji na wanamuziki kama vile Andrea
Vass na Luca Arosi, wote wamechangua kuongelea juu ya Injili moja kwa moja,hasa kwa
kutumia lugha ya sasa ambayo inapendelewa na vijana , kwa kumia nyimbo maarufu ziwe
kama zana kwa ajili ya kugundua uzuri wa kweli na wa kina.
Mwandishi wa Habari wa Radio Vatican alikutana na mmoja wa waanzilishi wa Tamasha
hilo ndugu Mdogo Matteo Della Torre anaye ishi katika Jumuiya mojawapo ya Brescia
nchini Italia na kusimulia juu ya mpango huo ulivyoanza.”Tumefikiria namna gani ya
kuoanisha Habari Njema na lugha ya kisasa ambayo inaeleweka kwa haraka na vijana,
kwa kuweka pamoja ngoma na muziki , pamoja na mawazo yetu ya hayo ni pamoja na kufanya
lugha iwe nzuri na mpya kwa vijana ambayo wanapendelea kuitumia , na katika kueneza
maneno ya Mungu”
“Kwa njia hiyo tamasha la unjilishaji linageuka kuwa muda wa sala kwa kuishi katika
mantiki ya ufunguo wa kileo ambapo vijana wanapenda kufanya uzoefu na hata kuanza
kujiuliza na kujitafiti wao wenyewe kwa namna ya kina”.Anapngeza,”kwa hakika siyo
kusema uzuri ni wa kushangaza tu kama tulivyozea kutazama na kusema bali, uzuri pia
unapaswa kumelemeta,kwa upande wangu ni jambalo linaloleta maana zaidi”.
Tamasha la kwanza la uinjilishaji limefanyika huko Rezzato Wilaya ya Brescia Desemba
mwaka jana .Vijana miambili waliweza kushiriki na kuwa pamoja kwa kutafakari, kutokana
na kwamba waliandaa tamasha hilo katika sehemu mbili ya kwanza ilikuwa inahus kutazama
uzuri wa kisanii kwa namna hiyo kwa kutumia rangi. Na sehemu ya pili ilikuwa inahusu
Biblia katika maigizo.Hiyo ni njia ya kuweka pamoja uzoefu binafsi wa maisha kwa kupitia
kurasa za Injili. Pamoja na hayo mpango huo ni tunda la utume wa wafranciskani kati
ya vjana ambao daima wamekuwa na tabia ya kusikiliza.
Hali kadhalika ndugu Matteo anafafanua zaidi akisema “hiyo ni kama safari ya kusindikizana
,kwa kufungua njia mpya ya maswali kwa vijana na pia kwa watu wazima wanao wakaribia
na kuzidi hata leo kutoa maswali yao.Ni njia mojawapo yenye nguvu ,na yenye maana
kwa mambo mengi yanayotokea.Kuwakaribia vijana ,unaona nguvu za mpango wa maisha
yao , ambao ki ukweli unataka kwa dhati kujitokeza katika mwanga. Kujiweka katika
safari na kutembea nao ni kuweza kuwasaidia wabadilike hata katika maswali yao , na
hata wakati mwingine ni kuwapokea tu jinsi walivyo.
Hata hivyo hata wao wenyewe mara nyingine wanajitambua maisha yao na ndani ya mioyo yao. Wana uwezo wa kutambua kwamba kuna mtu aliye na uwezo juu yao ya kuwafanya wapende maisha yao , hadi kuwafikisha baadhi ya uchaguzi muhimu.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |