2017-03-14 14:29:00

Jengo lenye uwezo wa nafasi ya mafunzo kwa vijana 570 Yeriko


Mafunzo ya sanaa,computa,maigizo na shughuli za michezo;ni baadhi ya shughuli ambazo zitatolewa bure katika kituo kipya kwa vijana kunzia miaka 14-29. Kituo kimezinduliwa wiki iliyopita huko Yeriko. Jengo limejengwa katika maeneochini ya usimamizi wa nchi ya Takatifu , kwa misaada kutoka Shirika la Misaada la  Marekani (USAID)  na  Shirika la kusaidia wakimbizi la Marekani (ENERA).Jengo lina uwezo w anafasi  570  kwa ajili ya kazi hiyo ya mafunzo na shughuli za wapelestina .Kwa maana nyingine ni kuwapa fursa vijana wa Yeriko kujiendeleza binafsi katika kutafuta namna ya kuingia katika nafasi za kazi.

Msimamizi wa kitume  maaneo Matakatifu anayo furaha kubwa ya kwamba, wanaweza kuweka uzoefu wao na kutoa huduma katika mipango kama hiyo;hiyo ndiyo mojawapao ya siri iliyowawezesha uwepo wao katika maeneo hayo kama wafranciskani ; ndiyo uwezo kutoa kuwa huduma kwa ajili ya wote.Ni maneno ya Padre Francesco Patton msimamizi wa eneo la Jumuiya ya Yeriko. Anasema,siasa ya kuwa wasimamzi wa maeneo hayo  haitoshelezi bali ni katika kuwatumikia jumuiya ndogo ya wakristo waliopo ambao  daima wanabaki Jumuiya ya ndogo ya kikristo  iliyo wazi kati ya waislam walio wengi.Kwa njia hiyo Kituo hicho kitapokea vijana wakristo na hata waislam kuwa shule ya watu wanaoishi pamoja.

Katika Hotuba yake Ndugu Mdogo Patton amesisitiza juu ya thamani ya elimu ya michezo na utamaduni. Naye ndugu mdogo Mario Hadchity ambaye ndiye mkuu wa  jumuiya ya Yeriko na Mkurugenzi wa Shule Nchi Takatifu , mahali ambao kituo hiki kimejengwa amesema, kwa miaka mingi sasa Jumuiya hizo zinatafuta kuwa daraja la amani , pamoja wamejishughulisha ili waweze kugeuka darala la uzuri, kwani uzuri ni jambo  ambalo linastahili kwa kila mtoto wa Mungu  pia ni jukumu la kuundeleza uzuri huo.  Mario anaongeza, kuishi katika mazingira mazuri na kuacha uzuri huo kwa wengine ni uwajibikaji.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kuswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.