2017-03-13 15:58:00

Kuna watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatari!


Karibia watoto 540 wakimbizi wasio sindikizwa na watu wazima au na wazazi wanaishi katika mji mmoja wa Melilla huko Hispania mpakani mwa nchi ya Morocco.Kati ya hawa ni mamia wanaishi barabarani na mitaani. Kutokana na taasisi kutokujali , walio wengi wanachezea maisha wakitafuta namna ya kusafiri kwa meli zinazotia nanga katika maeneo hayo .Watoto hao wanajigawa makundi na kuruka nguzo za waya  zinazotenganisha boma na mji wa Morocco  ili kutafuta namna ya kujificha katika mitumbwi na baadaye wanaogelee hadi wafikie Meli zinazokaribia kuanza safari zao. Hali hii inaitwa ni ya hatari na inaonekana kwamba watoto walio wengi ni  wasio kuwa na wazazi wao , wanaokimbia katoka maeneo ya wakimbizi walioko katika nyumba za makaribisho. Hiyo ndiyo njia pekee wanayofikiri ya kuwawezesha kutoka mji wa  Melilla  wafike  Bara la Ulaya.

Katika utafiti wa kukataliwa na kutelekezwa, hali ya watoto wanao lala barabarani  huko Milella, Chuo Kikuu cha Kipapa cha Camillas kimefanya utafiti na kutoa taarifa kuwa   katika kituo cha mapokezi cha La Purisima, kwa sasa kuna watoto 322 na vijana licha ya kwamba kituo hicho kinapaswa kuwa na idadi ya watoto 180 tu, na kwamba  vijana wengi wanalazima kulala sakafuni. Kwa mujibu wa takwimu katoka utafiti mwingine wa Harriage wanasema asilimia 92% za watoto wanaoishi katika vituo wanasema  wamepata uzoefu wa vurugu na mateso, na kwamba iwapo wanakimbilia mitaani na barabarabi ni kwa sababu ya kutafuta kuishi.

Licha ya kwamba uadilifu wa watoto hawa ni jukumu la Idara ya usalama wa Jamii na kituo cha La Purisima ,wanajikuta katika mazingira ya hatari na hasa katika mikono ya makundi ya mafia,vitendo haramu vya biashahara ya binadamu, madawa ya kulevya na pombe. Takwimu za hivi karibuni zilizotambuliwa na Shirika la “Karibuni wakimbizi” (Bienvenidos Refugiados) linasema taarifa ya watoto wahamiaji ni 540 wasio sindikizwa na watu wazima huko Melilla, hata kama wanasema ni idadi tu ya kukadiria. Kwa mujibu wa vyanzo vya takwimu  kutoka Idara ya Hifadhi ya Jamii, takwimu zisizo rasmi zinatoa taarifa kwamba mwaka 2016 waliingia watoto yatima wapatao 1,800  Melilla.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.