2017-03-11 16:58:00

Pongezi kwa Papa Francisko kwa kutimiza miaka 4 tangu achaguliwe !


Jumatatu 13 Machi 2017 Baba Mtakatifu anatimiza miaka 4 tangu achaguliwe kuliongoza Kanisa Katoliki la Mungu na katika tukio hili Kardinali Gerard Nichols ameandika Barua ya kumpongeza Baba Mtakatifu Francisko katika utume huo wa Khalifa wa mtume Petro. Barua hiyo inasema “tunamshukuru Mungu kwa utajiri wa zawadi na matunda ya Roho Mtakatifu, ambayo ndiyo yameongoza tabia ya utume wa Papa Francisko yaani  furaha , amani, uvumilivu , ukarimu , uaminifu , hekima na huruma.

Kardinali Nicholas  ambaye ni Rais wa Baraza la Maaskofu wa Uingereza na Gales anamshukuru sana Baba Mtakatifu kwa namna anavyojionesha , katika maneno , na matendo yake, katika mafundisho yake ya Kristo na Kanisa, anaongeza Kardinali Nichols “ mafundisho hayo yanaambatana na uhai na pia kueleweka haraka na hata kuleta mvuto kwa walio wengi duniani.Anasema, tumwombee  ili Mungu aweze kumpatia nguvu na ujasiri wa kuendelea na utume katika kiti cha Mtakatifu Petro.

Ikumbukwe kwamba, Baba Mtakatifu Francisko alichaguliwa tarehe 13 Machi 2013, akiwa mfuasi wa 265 wa  Mtume Petro. Aliingia madarakani mwezi mmoja wa kihistoria wa Kanisa Katoliki mara baada ya kung’atuka kwa Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita.Jioni ya tarehe 13 Machi Baba Mtakatifu Benedikto wa mi na sita alikuwa amemwambia yeye mwenyewe kwamba; tuanze safari  hii ya uaskofu na watu:Safari hiyo ya Kanisa la Roma, ambayo inatoa upendo kwa makanisa yote ya ulimwengu. Safari ya undugu na upendo na kwa matumaini katika Yesu. Tuombe kwa ajili yetu na kwa ajili ya wengine.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.