2017-03-11 17:15:00

Mazungumzo ni sehemu ya upendo na kuzidisha mahusiano hai ya mtu!


Jumamosi 10 Machi 2017, Baba Mtakatifu Francisko amekutana wanachama wa kujitolea wa simu chini Italia.Hawa ni watu wa kujitolea katika kusikiliza simu  ya rafiki nchini Italia , ambao wanaamini umuhimu wa kusikilizana pamoja na kujaribu kusaidia mahusiano kwa njia ya kusikiliza simu zaidi , ma kwa njia hiyo wanajibidisha kuleta ubora na utambuzi makini kwa wengine. Mara baada ya hotuba ya Rais wa chama hicho cha kujitolea katika kusikiliza simu Italia, ambapo wanaadhimisha  mwaka wa 50 tangu kuanzishwa kwake.

Baba Mtakatifu Francisko ametoa hotuba yake akisema kwa tukio la kuadhimisha miaka 50 ya chama chao tangu kuanza utume huo wa rafiki wa simu , umekuwa pia furaha na  mwafaka wa kukutana nao.Shughuli zenu za kuwasaidia wale wanao ishi upweke , wanahitaji kusikilizwa, na masaada wa kiutu.Ni huduma muhimu , na zaidi kwa nyakati za sasa ambayo inakabiliwa na changamoto ya nyingi ambazo pia ni chanzo cha ule upweke na ukosefu wa mawasiliano.Katika miji mikubwa, pamoja na kujaaa watu wengi, lakini maisha yake yanaonesha kutawalia na ubinafsi:kwa mfano wa utofauti unao kithiri,mawasiliano  zaidi kupitia mitandao ya kijamii (igitali) badala ya mawasiliano ya mtu moja kwa moja , upungufu wa mishahara ya kuweza kukidhi mahitaji muhimu, utamaduni wa kujionesha wanazo au kutaka kuonekana .Baba Mtakatifu Francisko anaongeza katika mantiki hizi ni lazima kuzingatia na kusisitiza uwepo wa  mazungmzo na kusikiliza.

Mazungumzo yanasaidia kutambuana , na kuwelewana pamoja hata katika mahitaji.Hawali ya yote ni sehemu ya kuonesha heshima kwasababu inawaweka watu katika hali ya kujifunua kila mmoja kwa kutambua mambo msingi ambayo yanaweza kushirikishana.Na zaidi mazungumzo pia ni sehemu ya upendo , kwasababu pamoja na kuweka pembeni dhararu za utofauti , inaweza kusaidi kutatua matatizo, na kuweza kushirikishana hatua mbalimbali kwa manufaa ya wote.Kwa njia ya mazungumzo , tunaweza kujifunza kutazama , mwingine bila kuwahukumu au kuwaona kuwa siyo adui bali ni kumwona kama zawadi ya Mungu, anaye tuhimiza kutambuana.Mazunguzo yanasaidia watu wazidishe mahusiano ya kibinadamu na kushinda vizingiti vya kutokuelewana.Kama kungekuwapo na mazungumzo ya kweli katika familia, maeneo ya kazi , katika sera za kisiasa, mambo mengi yangeweza kutatuliwa kwa urahisi.Hali ya kuwa katika mazungumzo inahitaji uwezo mkubwa  wa kusikiliza, lakini kwa bahati mbaya Baba Mtakatifu anasema hiyo haipo kwa watu walio wengi.

Katika kumsikiliza mwenzako inahitaji uvumilivu na umakini.Ni kwa yule tu  anayetambua  kunyamaza, anajua kusikiliza: kumsikiliza Mungu na ndugu kaka na dada anayehitaji msaada, kusikiliza rafiki na familia.Mungu mwenyewe ni mfano halisi wa kusikiliza: mara zote tunapokuwa tunasali,yeye mwenyewe anasikiliza , bila kuomba jambo lolote , na zaid ni yeye anaye anza kuomba kwa ajili yetu,(Furaha ya Injili 24, ) katika kusikiliza maombi ya msaada wetu.Tabia ya kusikiliza ndiyp pia Mungu mfano inatuhamasisha kupambana na kuta za kutokuelewana, na kujenga madaraja ya mawasiliano, kwa kushinda upweke na kufungua njia katika ulimwengu binafsi.Baba Mtakatifu Francisko anasema, kwa njia ya kusikiliza , inawezekana kuchagua kujenga ulimwengu ulio bora, na kufanya matendo ya makaribisho na heshima,kwa kupinga mgawanyiko na misukosuko.Anawatia moyo waendelee kwa moyo wao wote katika juhudi za huduma yao msingi katika jamii, kwasababu hasiwepo hata mmoja anayebaki pweke, na pia bila kuvunja mnyororo wa mshikamano katika mazungumzo .Kwa maana ya kwamba kamwe isikosekane hali ya kusikilizwa ambayo ndiyo ishara halisi ya upendo wa dhati kwa ndugu.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radi vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.