2017-03-10 17:38:00

Sauti ya nguvu ya Yesu msalabani hakuita Elia bali Baba yake!


Katika msalaba Yesu anaweka ubavu wake ambao baadaye utamwaga maji na damu,kwa ajili ya msamaha wa dhambi , hayo ni mojawapo ya tafakari imeongoza Padre Giulio Michilini wakati wa Mafungo ya kiroho sehemu ya saba kwa Baba Mtaktifu Franciko na  Sekratarieti yake huko Ariccia.Mtazamo wa kina wa upendo  wa Yesu msulibiwa , amabo Padre Michelini amefanya katika takari la saba kwa kutazama kifo cha masiha katika Injili ya Matayo akitamka kwamaba ni kifo cha kweli na siyo cha kijuu juu. Siyo kwamba mitume walitaka kusita juu ya kurudia maisha yake , bali ni tendo la ukweli kwasababu Yesu alikufa kweli kweli.Habari zinazoeleza juu ya kifo cha Yesu siyo nzuri ni za ukatili mkubwa kwa mfano kilio chake akiwa msalabani, ambacho mara nyingi imedhaniwa  kuwa ni kilio cha kutia aibu , lakini siyo habari ambazo ziliundwa tu, bali ziandikwa kwasababu ya kueleza ukweli wa jambo fulani lililojitokeza. Hawali ya yote zinapaswa kuchambuliwa  kwa maana ya majaribu ambayo Yesu alijisikia katika msalaba , na hasa anapotamka Mungu wangu Mungu wangu mbona unaniacha,hiyo hata wale wa kuwa wanatazama ukatili huo hawakuweza kutambua mateso ya Kristo. Padre Michelini anasema hiyo inathibitisha katika Injili zinazofanana ya kuwa watu hao walifikiri Yesu anamwita Elia.

Je alikuwa nani huyo Elia waliyedhania Yesu anamwita? Kwa hakika walifikiri ni nabii ambaye angerudi, lakini angeweza kufanya jambo gani,?La kumwondoa Yesu  kutoka msalabani.Au kama tunavyosoma katika Injili ya kuwa Elia ameshakuja , na pia kwa njia ya Yohane  Mbatizaji? Alikuwa akimwita rafiki yake .Kwa namana moja , ni baadhi ya maswali ambayo hawakuwelewa , kwasababu Yesu hakuwa namwita Elia na wala Yohane Mbatizaji kwa sauti ya nguvu Yesu alikuwa anamwita Baba .Ila Baba mwenyewe amenyamaza.Tendo la Baba kutokusikika katika hilo, Padre Michelini anasema ni kipingamizi cha simulizi nzima ya kifo cha Yesu.Fikra za Yesu alizo nazo kwa muda huo, kwa maana ya kuachwa peke yake na Baba , kwa namna nyingin inaongeza jambo la aibu kweli  kwani ni kutaka kuonesha ugumu wa kubuni.Lakini  Yesu analalamika kweli lakini siyo kwamba anajisikia kuachwa na Baba yake, au kwa ajili ya maumivu, bali analalamika kutokana  kuishiwa nguvu za kimwili.Pamoja na hayo Injili ya Yohane na Luka hawaelezi kifo cha Kristo msabalani, kwasababu Padre Micheli anaongeza ya kwamba kwa upande wao  ni jambo la aibu kubwa.

Mateso ya maisha ya Yesu ambayo hayakuelewaka, hata akiwa msalabani , Padre Michelini anasema ni jambo la kushangaza sana .Lakini kwanini hawaelewi? kwa kutambua hili  inahitaji uzoefu binafsi ,akitoa mfano mmoja  wa wanandoa walio kuwa na matatizo yao,matatizo yaliyo sababishwa na mke kugundua ujumbe wa kusalitiwa katika simu ya mume wake,kwa namna hiyo kati yao ulitokea mpasuko mkubwa wa kutokuelewana katika ndoa yao.Hata kama ukieleza namna gai kwa upande wa Yesu ni vigumu kueleza wakati yuko msalabani. Padre Michelini anasema kwetu sisi tunatambua ya kwamba msalaba unaeleza kila kitu .Lakini kwa upande wa Yesu huwezi kusema alikuwa namwita Elia,anachoweza kufanya ni kuamini roho ambaye baadaye ndiyo itakuwa zawadi kutoka kwake ,ili Roho iweze kueleza kila kiui ambacho tunashindwa kuelewa.Hiyo lakini itabidi kusubiri ufufuko  na kukaa  mitume mezani kwa siku 40,ni maelezo tunayo soma katika kitabu cha matendo ya mitume, kwaajili ya kuwandikiza mitume ambao hawaelewi kitu.

Padre  Michelini pia anakumbuka katika matukio haya ya mwisho ya mateso ya mshale wa askari .Akikumbuka matukio ya Kafarnaum , ya kwamba askari alikuja kumuomba msaada wa mtoto wake aliye kuwa naaumwa. Na Yesu hakukataa ishara yake ya upendo.Lakini kwa sasa katika Injili ya Matayo inaeleza kwamba Askari anatoa mkuki , na Yesu anamgeuzia shavu jingine , kama alivyo kuwa amefundisha wanafunzi wake kule mlimani.Huko Kafarnamum alimpatia Askari fursa kwa mara nyingine tena: lakini sasa mbele ya msalaba anaweza kumgeuzia ubavu wake ambao utatoka Maji na Damu kwa ajili ya msamaha wa dhambi.Na mwisho Padre Michelini anatazama wanawake walio kuwa pale  msalabani:kati yao kulikuwepo na Maria mama wa Yakobo na Yosefu , nakusema  wengine wanatafsiri alikuwa ni mama wa Bwan wetu Yesu Kristo aliyekuwapo chini ya msalaba. Anawaalika wajiulize kama mioyo yao imefungwa kwasababu ya kiburi,hawataki na wala kuwatambua  wengine. Anatoa wito wa kutafuta kujua zaidi mabaya yao na kufanya mawasiliano na wengine kwa kuboresha, na kukua katika unyenyekevu . Kwa njia hiyo wanaweza kutambua uwepo wa Mungu katika maisha yak ila siku na hata kwa mtazamo wa wengine.

Hali kadhalika Katika tafakari sehemu ya 6 ya mafungo ya kiroho Padre Michelini anawatafakarisha juu ya mchakato wa Yesu mbele ya mke wa Pilato (Mt 27,11-26).Padre Michelini anatumia tafakari zilizoandikwa na wanandoa Mariateresa Zattoni na Gilberto Gillini ambao kwa miaka mingi wanashirikiana nao katika tafakari za mafunzo ya kiroho kwa familia, na mikutano mingi ya mafunzo ya kiroho.Padre Michelini anasema;masomo  na takafakari ya neno la Mungu haikuwekwa kwa ajili ya watawa au wahusika wengine , bali hata wana ndoa na familia wanapaswa kusaidiwa ili wapate kuweka katika matendo, jambo ambalo anasema had sasa linaonekana kutoliwa mkazo na Kanisa.Hawali ya yote Padre ametafakari juu ya maamuzi ya Ponsio Pilato , kati ya Yesu una Baraba ,na kukumbusha tafsiri iliyotolewa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto wa kumi sita juu ya waandishi wa kizamani kama Origene kwa jina la Barabba na pia Yesu.Hali kadhalika katika tafakari hilo anaonesha juu ya umuhimu wa kuona mwijili Matayo kuhusu umuhimu wa Damu ya Yesu kwa ajili ya msamaha wa dhambi.Anasema mantiki hiyo ya kiteolojia iliyo oneshwa na Matayo isiweze lakini kupoteza maana kubwa ya binadamu , kwasababu jambo lilotokea kwa watu wawili mbele ya Pilato likuwa halijawahi kutokea.


Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.