2017-03-09 11:48:00

Askofu mkuu Charles John Brown ateuliwa kuwa Balozi Albania


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Charles John Brown kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Albania. Kabla ya uteuzi huu, Askofu Brown alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Ireland. Itakumbukwa kwamba, alizaliwa tarehe 13 Oktoba 1959, huko New York, Marekani. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 13 Mei 1989 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kunako tarehe 26 Novemba 2011, akamteua kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini Ireland. Kunako tarehe 6 Januari 2012 akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.