2017-03-08 17:07:00

Chiara Lubich:Karama ya huduma ya umoja wa familia ya Mungu


Tarehe 14 Machi 2017 itakuwa siku ya kukumbuka miaka 7 ya kifo cha Chiara Lubich, Mwanzilishi wa Shirika la Kitume la Wafokolari.Katika kuadhimisha kumbukumbu ya kifo chake,wameandaa mkutano utakao husu mada ya familia kwa  maongozo wa Sinodi ya Familia katika kujikita zaid na tafakari juu ya wosia wa Baba Mtakatifu Francisko "Furaha ya Upendo".Pamoja na maadhimisho hayo yanakwenda sambamba na miaka 50 ya kuanzishwa kwa Shirika hilo mwaka 1967 hilo ambalo limeenea duniani kote.Katika maisha ya Chiara alikuwa akiona ndani ya familia kama mbegu ya umoja kwa ajili ya binadamu wa milenia ya tatu.Na katika ujumbe wake wa matashi mema sikukuu ya Familia kwa mwaka 1993 alisema thamani ya familia ni asili ya zawadi ya bure, kwani ni roho ya huduma na ya kushirikishana ambapo wanafamilia  wanaweza kusambaza tunu hizo kwa familia nzima ya binadamu.

Ni kutokana na ufunguo huo, ya kwamba jumuiya ya Wafokolari kwa mwaka 2017 walio sambaa dunia nzima wataweza kutafakari. Lengo lao la mwisho ni kujikita katika safari ya maisha na fikra zao kwa miaka hii 50 ya shirika lao na kuifanya iwe na thamani na mwanga wa binadamu katika ulimwengu wa familia kwa mtazamo wa upeo wa  juu wa binadamu kwa ujumla.Tukio la kwanza juu ya mada Familia ni chanzo cha matumaini na furaha, lilifanyika mjini Cairo Misri ikiwa na washiriki 300 :palikuwepo na mipango ya sherehe na shuhuda , ambapo fursa za vijana zilionekana kupewa kipaumbele na mahusiano katika ya kizazi ndani ya familia.Vile mkutano mwingine ulikuwa huko Panama pia kuhusu mada ya familia , ambayo ilifanyika tarehe 12 Februari 2017 kuhusu jamii inayoonesha tabia za haraka ya maisha. Zaidi ya watu 400 waliweza kukutana katika uwanja mkubwa wa wazalendo kwa siku ya mjadala , michezo na matembezi.

Tukio hili la ulimwengu litapata kuadhimishwa katika makao makuu yaliyoko huko Loppiano Firenze Italia  kwa kuanza na  mikutano tarehe 10 hadi 12 Machi 2017 , familia nzima ya wafokolalini kutoka mabara yote matano. Kutakuwepo na mipango mingine ya mikutano ya wazazi , watoto, na wazee. 
Pia makundi ya wataalamu mbalimbali, wataweza kuwapa semina kuhusu Mkataba wa usawa katika maisha ya familia, namna ya kujiamni na mahusiano.Mafundisho hayo yatafanyika kwa ushirikiano wa Taasisi ya Chuo Kikuu Cha Sophia, kwa lengo la kuimarisha mchango wa kiroho wa umoja kwa ajili ya familia leo hii.

Tukio kuu na lenye maana zaidi huko Loppiano litakuwa na fursa  alasiri ya Jumamosi  tarehe 11 Machi 2017 ambapo itakuwa imegawanyika katika sehemu tatu kuu,familia na mtandao wa mahusiano,mahusiano ndani ya ndoa, na  watoto wao, kati ya vizazi; Sehemu ya pili itakuwa Upendo ni  chombo na majibu ya kukabilina na masuala muhimu katika famili kwa kushirikishana majeraha , changamoto , huzuni.Familia kama rasirimali ya ubunifu katika masuala ya kijamii kwa kila mtu ambapo lengo ni kutazama mitandao ya familia, mshikamano na ukarimu,pia  kujitolea kwa jamii.
Ili kuweza kufanikisha ratiba hiyo watatumia njia ya ubadilisha hadithi za kweli za familia katika ushuhuda .Hizo ndizo tafakari zenye sifa na mchango mkubwa utokanao na urithi wa utamaduni wa fikra za Chiara Lubich juu ya Familia.Kila mwaka, maadhimisho ya kifo cha Chiara Lubich kwa jumuiya Fokolari duniani inawapa fursa ya kukutana, ya sikukuku, ya ushuhuda na marudio ya uwajibu wa utume wao  kwa upya .

Kwa mwaka 2017, mikutano imeongezeka mara dufu ambapo itaona Singapore, Vilnius (Lithuania), Sydney(Australia) ,Houston (USA), Manaus (Brazil),. Bujumbura (Burundi).Kwa namna ya mzunguko huo wa dunia ni kuthibitisha maneno ya Mama Chiara yasemayo “ninyi ni familia moja”

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.