2017-03-07 16:41:00

Hatuwezi kuacha watoto na wajukuu zetu waangukiwe na nyuklia


Shule ziwe nyingi badala ya nyuklia na zaidi bora juhudi za kiuchumi kwa ajili ya mafunzo ya elimu ya vijana badala ya kuwapo fedha za uwekezaji katika maendeleo ya nishati inayodhaniwa kuwa hatari katika ulinzi wa mazingira kwasababu inalenga juu ya nishati ya nyulia.Hii pia ni katika mtazamo wa kuepuka maendeleo zaidi ya nguvu mbadala na endelevu. Ni wito uliotolewa na Askofu Mkuu wa Kianglikani Thabo Makgoba wa Afrika ya Kusini hivi karibuni kwa Serikali ya Afrika ya Kusini , ili wasitishe juu ya tangazo la hatua ya maendeleo ya nyukila.Tamko lillofuatia maandanamo ya hivi karibuni na makundi ya utetezi wa mazingira ambao wanaomba kusitisha mipango hiyo ya nishati ya nyuklia inayo chukuliwa kuwa haina maana na yakutoa  madhara tu. Hata hivyo Jumuiya ya waangilikani wameingilia kati kutokana uzoefu  wa muda mrefu sasa wa mpango wa kijani.

Gazeti la Newa Service linasema Askofu Mkuu Makgoba ameakilisha suala hili katika Sinodi ya Waaangilikani wa Afrika ya Kusini walio kutana hivi karibuni huko Benoni eneo karibu na Mji wa Johannesburg. Katika tukio hili Askofu huyo anasema msimamo waao na kuonesha katika Sinodi yao ya Jimbo iliyofanyika Septemba mwaka Jana ambayo tayari walionesha upinzani wa upanuzi wa nishati ya nyukilia na kuitaka Serikali kujiingiza katika njia ya maendeleo ya nishati mbadala.Kwa maana hiyo Askofu Makgoba anakaribishwa hatua zilizochukuliwa hivi karibuni na Rais Jacob Zuma katika suala la kendeleza nishati ya kijani kwa kuzingatia vyema juu ya maendelea chanya  kauli juu ya maendelea kidogo  ya nyuklia kwa madai ya mahitaji ya Taifa.
Hata hivo Askofu Mkuu wa Kianglikani anabainisha kuwa haitoshi , nyuklia inapaswa iondolewe kabisa katika ajenda ya maendele ya taifa leo, ambapo kwa sasa ni sehemu ya mpango wa kati ambao unatazamiwa kwa mwaka 20137 , mwaka ambao Afrika ya Kusini lazima kufikia mojawapo ya maendeleo.Lakini tangu lini anasema upeo wa nishati ukafikia thamani yake na zaidi kuleta faida kuliko ilivyo sasa ya kufanya uwezekano wa maendelo ya nyuklia?

 Kama ilivyo kuwa imesha tolewa mwaka jana  barua iliyotumwa kwa Rais Zuma , maaskofu wa Kiangliani wanafikiria kwamba zipo fursa nyingine  za kupewa kipaumbele katika nchi hiyo kama vile  kuanzia maendeleo ya elimu kwa wote, pia ongezeka kubwa la hali ya wastani wa maisha ya wanachi wote ambao leo hii wanateseka kwa mateso kwa mambo mengi.Kwa njia hiyo gharama kubwa na mikopo inayohusiana na mahusiano ya nishati yanafikiriwa ni vitu visivvyo na maana kwa sasa katika nchi inayo endelea kutafuta marakwa mara utulivu na uchumi wa kudumu.
Kwa namna hiyo wanasema wana wasiwasi mkubwa kwamba kupanua mpango wa nyuklia unaweza kuwakilisha kitu zaidi ya upanga juu ya vichwa vya watoto wao na wajukuu wao.Wanasema hawawezi kuacha vizazi vijavyo watupiliwe mzigo wa taka za nyukilia.Wanaamini kwamba Afrika ya Kusini ina uwezo wa kuweza kuwa na nishati mbadala, ikawa kitovu cha bara zima na uwezo mkubwa kwa ajili a ukuaji wa uwekezaji katika uzalishaji na katika nguvu kazi.

Ikumbukwe kwamba hayo yasemwayo na Afrika ya Kusini ni mojawapo ya matatizo yanayoikabili bara zima ambayo tayari jumuiya ya Kiianglikana iko katika kazi ya ulinzi wa Mazingira. Kwa mfano siku chache zilizopita nchini Burundi na fursa ya uwepo wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kianglikana Justin Welby, walifungua kampeni ya mpango wa kupanda miti milioni 10

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahli ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.