2017-03-06 16:28:00

Tuwe na mazoea ya kufungua Biblia muda wote tupate kuangazwa


Ujumbe wa kuwa na mazoea ya Biblia kama simu ya mkononi  ambayo ni maneno aliyo yatoa Baba Mtakatiu Francisko wakati wa sala ya Malaika , akisisitiza juu ya umuhimu wa Neno la Mungu unavyo paswa kuwa nao katika maisha yetu ya kila siku umekuwa ndiyo mazungumzo katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii duniani. Baba Mtatifu kwa mara nyingine tena ameweza kutoa ujumbe muhimu kwa kutumia lugha inayojulikana kwa wote. Katika kutoa somo juu ya mawasiliano ya Baba Mtakatifu Mwandishi wa habari wa Radio Vatican alimhoji Profesa Chiara Giaccardi wa somo la Jamii ya machakato wa utamaduni na mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Milano na kusema ;Baba mtakatifu ametuzoesha sasa kutoa mafundisho makubwa ya mawasiliano na hasa uwezo wa kugusa kile cha moyo, yaani yale ambayo tunatambua kabisa kwasababu ndiyo yanayotukabili kila siku.

Mwandishi mmoja Goette anasema mambo tunayo yapenda, yanatubadilisha na hivyo kwa muda huu tunapenda mambo ya teknolojia.Kwa njia hiyo mafundisho yake na misemo yake kuanzia kwenye teknolojia inayo tuzunguka kwa sasa, lazima ielewake zaidi.Baba Mtakatifu anataka kuchangamotisha kwamba  vitabu na mambo ya kidigitali siyo vitu viwili tofauti bali ni mambo ambayo yanaweza kwenda sambamba, la muhimu kujibidisha katika maisha yetu ya kila siku.Baba Mtakatifu Francisko wakati wa sala ya malaika wa bwana ameuliza swali  mahujaji wote a waamini ya kwamba ni nini kinaweza kujitokeza iwapo ujumbe wa Mungu unaweza kusomwa kila wakati kama vile usomwapo ujumbe wa simu za mikono ,hapa  ikiwa na maana ya taadhali kubwa , ya kweka Mungu katikati katika maisha ya mkristo kwa njia hiyo Profesa Giaccardi,anahijiwa akilini na mwandishi mmoja McLuhan juu ya Biblia na mapinduzi ambayo yalitokea  kuanzia kitabu kilichopishwa, hata kufikia katika computa na  Ipad , ambapo kila mmoja anaweza kujongea na kujisomea binafsi . Pamoja na hayo mapinduzi haya sasa yamezidi kuongezeka kufikia hatua ya digital.Ni kweli kwamba kama maneno hayo tunayo ambatana nayo kila siku  tungeweza kusoma , ni hakika mapinduzi mapya yangeweza kutokea katika maisha yetu , kwa namna hiyo   Papa anatualika kwa dhati kufanya hivyo. Anasisitiza Profesa.

Aidha anaongeza ,Baba Mtakatifu Francisko anasema  kwa sasa kila kitu kinaruhusiwa , lakini dini siyo kitu cha kuunda kwamba Jumapili ni kwenda katika misa kusali au kwenda chumba cha faragha mwenyewe , bali ni Neno la Mungu ,na  kitu ambacho kinatusindikiza katika maisha yetu yote kwa kutoa fursa za kufungua madirisha tofauti.Kwa mfano ujumbe wa Baba Mtakatifu Benedikto wa XVI wa Siku ya 47 ya Kimataifa ya  mawasiliano alipozungmza juu ya vyomboo vya habari kama milango.Kwa  kupitia madirisha hayo sisi tunaweza kuangalia hali halisi kwa njia moja na tunaweza kuwa na mtizamo mpya na wa uhuru. Hivyo Kama  Baba Mtakatifu Francisko  anavyosisitiza kwamba Biblia siyo mlolongo wa sheria bali ni dirisha ambalo uruhusu hewa mpya kuingia na kutufanya tupumue na tuwe huru zaidi kutokana na vikwazo vingi vya maisha yetu ya kila siku.

Hata hivyo Aprili 2014 Baba Mtakatifu Francisko aliyasema pia  maneno kama hayo ya kwamba unaweza kusoma hata  Injili kwa kupitia vyombo vya kiteknoloija ,kwani kwa sasa  Biblia nzima unaweza kuipata kupitia katika simu za mikono , tablet na kusisitiza namna ya teknolijia inavyo weza kusaidia katika neno la Mungu. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko kwa mara nyingne tena anatoa changamoto kwetu sisi ya kwamba Neno la Mungu siyo kitabu cha kuweka ndani ya kabati chumbani  na kuhifadhi bali inafaa zaidi Biblia kuwa kifaa cha kuweka kwenye mifuko yetu ambapo muda wowote unaweza kufunua na kuangazwa . Profesa anaongeza ,hiyo ndiyo njia ambayo Baba Mtakatifu anatuhimiza tuwe na mazoea badala ya kuepuka kwasababu ni njia mpya inayotupatia uhuru iwapo tutaweza kufungua milango ili Neno la ukweli lipate kuingia. 

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.