2017-03-04 10:11:00

Kanisa la Mungu katika mchakato wa kuwapata wenye heri wapya


Baba Mtakatifu Francisko hivi karibuni amekutana na Kardinali Angelo Amato (S.D.B), Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya kuwatangaza waamini kuwa wenyeheri na watakatifu na kuridhia maombi yaliyowasilishwa kwake ya kuwatangaza wenye heri watumishi wa Mungu: Tito Zeman, Padre wa Shirika la wa Salesiani la Mtakatifu John; alizaliwa 4 Januari  1915 na kuuwawa kwa ajili ya utetezi wa iamani yake 8 Januari 1969;Pia -Mtumishi wa Mungu  Ottavio Ortiz Arrieta Shirika hilo la Mtakatifu John Bosco Askofu wa  Chachapoyas; alizaliwa 19 Aprili 1878 kifo chake tarehe  1° Machi 1958;

Mtumishi wa Mungu Antonio Provolo, Padri wa Jimbo na Mwanzilishi wa chama cha Maria na kwa ajili ya mafunzo ya vizi na Shirika la Maria kwa ajili ya kufundisha viziwi ; alizaliwa  17 Februari 1801 na kifo chake 4 Novemba 1842; Mtumishi wa Mungu Antonio Repiso Martínez de Orbe,Padri wa Shirika la Wajesuiti, mwamzilishi wa Watawa wa kike wa Mchungaji mwema ;alizaliwa 8 Februari 1856 na kifo chake  27 Julai  1929. Mtumishi wa Mungu  Maria della Mercede Cabezas Terrero, Mwanzilishi wa Shirika la Kimisionari la wafanyakazi wa Moyo Mtaktifu wa Yesu ; alizaliwa 19 Desemba 1911 na kifo chake 30 Septemba 1993.

Mtumishi wa Mungu  Lucia wa moyo safi wa Maria wa Shirika la Watoto wa msaada ; alizaliwa 26 Mei 1909 na kifo chake  4 Juni 1954; Mtumishi wa Mungu Pietro Herrero Rubio, Mlei ;alizaliwa 29 aprile 1904 na kifo chake  5 Novemba 1978;  Mtumishi wa Mungu Vittorio Trancanelli, Mlei  na baba wa Familia alizaliwa tarehe 26 Aprili 1944 na kufariki dunia 24 Juni 1998.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.