2017-03-02 13:55:00

Siku ya Kimataifa ya magonjwa Adimu "kwa utafiti upo uwezekano"


Kwa utafiti , upo uwezekano usio kuwa na mwisho, ni kauli mbiu ambayo imeongoza mwaka huu katika Siku ya Kimataifa ya magonjwa Adimu, iliyo fanyika 28 Februari 2017.Kwa upande wa nchi ya Italia ni wagonjwa zaidi ya 600,000 hali ambayo imeifananishwa na kikundi cha wanajeshi. Kwa mujibu wa Shirikisho la TUUNGANE nchini Italia wakiwa pamoja na Taasisi nyingine tatu za Afya wameandaa wiki ya matukio kwa ngazi zote ili kuongeza ufahamu na kuhamasisha  wote kujenga mtandao wa kuwazunguka wagonjwa kwa maana ya kuwasaidia.

Kujua ni magonjwa yapi Adimu na matokeo yake, ndiyo lengo kubwa la siku ya Kimataifa ya magonjwa nadra  kwa sababu wagonjwa walio wengi na wasio onekana , wapate kujua mahitaji yao wazi kwa kutafuta ufumbuzi wa uhakika na kutosha.Magonjwa nadra kwa asili hayaonekani , kiasi cha kutokea mtu mmoja kati 2000.Na magonjwa haya yapo kwani takwimu nchini Italia zinaonesha kuwa ni wagonjwa karibia 7000, ambapo ni asilimia 80% yenye asili kutoka Italia.“Magonjwa nadra yanayo julikana hadi sasa ni karibia 195,000 kwa mujibu wa takwimu ya Taasisi ya juu ya Afya nchini Italia.Magojwa ya asili , na yasiyo ya asili, yanaleta pia ulemavu na Magonjwa hayo nadra mara nyingi hubadili namna ya kufikiri na hata matibabu yake, hayo yana dhibitishwa na Daktari Giuseppa Zampino  Mhusika wa kituo cha Magonjwa nadra na watoto wanao zaliwa na kasoro cha Hospitali kuu ya Policlinico Gemelli mjini Roma Italia.

Kama mtoto amezaliwa na kasoro, kuna mahitaji ya sera za afya kijamii , ili kusaidia wagonjwa na familia zao.Pia kuna magonjwa sugu , ambapo kuna haja ya kuhusisha madawa ya mtoto na madwa ya mtu mzima, pia mzee.Ni hali ya utata sana kiasi kwamba kuna haja ya kutambua maarifa , ili kuufikia mkakati anasisitiza,na kusema kwakuwa unaingilia hata ulemavu bado kuna haja kubwa na  tahadhari hasa kwa kutazama aina ya jamii na binadamu ili wagonjwa wasijisikie kuwa na upweke. 
Daktari Zampino anaongeza kuelezea juu ya utata katika utafiti , akisema kwamba ili kufika utambuzi wa magonjwa adimu unaweza kuchukua hata miaka mitatu na nusu kutokana na utamaduni mdogo kwa upande wa matumizi ya madawa kwa ujumla, kwasababu ugonjwa huo unaweza kujitokeza wazi baada ya kupindi kirefu na hali pia ni tofauti sana.

Hali kadhalika anasema kuna hali mbaya ambayo ìnayohitaji kuishi kwa masharti,na hata aina nyingine ya magonjwa nadra ambayo haina vikwazo vyovyote kwa mfano mtoto ambaye amepatwa na ugojwa uitwao Noonan ambao aiungiliani na matatizo ya moyo , anaweza kuishi maisha ya kwaida.Lakini kuna ugonjwa mwingine ambao ukimpata mtu , anaishi kwa hali ya vikwazo kutokana na viungo vya mwili kupoteza nguvu zake taratibu hadi kufikia mauti.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.