Maombi ya msaada wa kifedha kwa ajili ya ujenzi wa mji na vijiji vya Piana na
Ninawi ,mahali ambapo wanaishi wakristo walio kimbia vita vya wana jihadi wa dola
ya Kiislam(Daesh) kati ya mwezi Juni na Agosti 2014.Maombi hayo yametolewa na Patriaki
wa Wakaldayo kwasabu watu wake na wa jumuiya ya jamii nyingi waliacha ardhi yao ya
jadi na kusambaa katika maeneo mengi ya dunia.
Maeneo ya kipatriaki na baadhi ya majimbo fulani tayari wamekusanya karibu milioni
500 dinari za Ira zenye thamani ya uro zaidi ya 380 elfu, ili kuharakisha ujenzi wa
nyumba na makanisa yaliyo haribiwa wakati wa miaka ya vita vya kijihadi, kwa kufanya
hivyo ni kuruhusu watu warudi wale wanao pendelea kurudi majumbani kwao.
Katika maombi ya Patriaki amewataka jumuiya zote kuendelea kusaidia kwa ukarimu mipango
ya ujenzi kama walivyo kwisha fanya wakati wa kuwasaidia wakimbizi walio kimbia vijiji
vya Ninawi .Taarifa inasema kwa njia hiyo waweze kuwahakikisha wale wanao taka kurudi
nyuma wafike kabla ya kuanza mwaka ujao.Halikadhalika ujumbe wa Partiaki wa kaldayo
unatoa taadhali kwa waaangalizi wa kimataifa. Ni kwa dhamana ya kufuatilia kama inawezekana
kutokea ukiukwaji na kuleta migogoro kutoka kwa vikosi vinavyoshiriki vita dhidi
ya majeshi ya kijihadi .Pia kuzuia mapigano baina ya serikali kuu na mikoa ya serikali
ya Kurdistan ya Iraq katika mwelekeo wa kisiasa na utawala wa maeneo yaliyo chukuliwa
hawali na wanajihadi.
Patriaki anasisitiza juu ya haja ya kuhusisha watu katika machakato wa ujenzi na makundi
wa wenye sifa ambao wanatenda kwa moyo wa ukarimu na mshikamano bila kufuata maslahi
yao binafsi.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |