2017-02-27 15:25:00

Wasiwasi wa Maaskofu wa Jamhuri ya Dominika juu ya vijana


Vijana wadogo na wakubwa katika hali halisi ya nchi ya Dominika.Ni ujumbe wa Mkutano wa Baraza la maaskofu wa Jamhuri ya Dominika uliotolewa kwa tukio la 173 la kuadhimisha Sikukuu ya Uhuru, tarehe 27 Februari 2017. Nchi ya Jamhuri ya Dominika iko kwenye kisiwa cha Bahari ya Karibi cha Hispaniola inayopakana na nchi ya Haiti.Tunataka kushiriki na kila mtu kutoa wasiwasi kuhusu hali halisi ya vijana wadogo na wakubwa katika nchi ambapo asilimia 36,3% ya wakazi wote wa nchi ya Dominika imeundwa na vijana kati ya miaka 10 na 29, katika wao kuna maadili mengi ambayo uwapa matumaini ya baadaye, kama vile juhudi katika kujifunza, uwezekano wa kutengeneza matukio ya sikukuu , furaha hata katika matatizo ya sasa, tabia ya kukusanyika na kuimarisha urafiki,zaidi vijana wengi wanafanya kazi kuonesha ubunifu  katika hisia za ujasiriamali,zaidi vijana wetu ni wakarimu na wenye kuwa na mshikamano katika jumuiya yetu, wanasema maaskofu.

Ni vijana wengi wanao mtafuta Bwana katika Kanisa katoliki na hata katika jumuiya nyingine za Kanisa,wakiwa pamoja katika makundi ya vijana , na kutoa huduma katika mafundisho ya katekisimu , liturjia na hata huduma nyingine za kijamii.Halikdhalika umekuwepo ongezeka la miito ya kikuhani na miito katika maisha ya utawa,hata katika huduma nyingine za vyama vya walei.Maaskofu wanasema pamoja na ukosefu wa usawa wa kijamii, kiuchumi na kiutamaduni ulioko kati yetu, sehemu kubwa ya familia ,inawasaidia vijana katika masomo yao na katika maendeleo ya binadamu na kikristo katika changomoto kubwa zilizopo ndani ya nchi.Maaskofu wanaeleza uchungu wao wa nchi yao, kutokana na kwamba watoto wengi wanazaliwa mahali ambapo inakosa picha ya baba au mama ambaye anaweza kuwaongoza watoto  hao mahali ambapo ugonvi ndani unazidi kuwa wa hali ya juu.Umasikini unaikumba nchi ya Jamhuri ya Dominikani kwa asilimia 40% ya familia,na kusababisha ukosefu wa usawa, pia kupunguza fursa za  kustahimili masomo hata maendeleo ya maisha.Viongozi ni adimu kijamii na kisiasa ambao wanaweza kweli kuhudumia watu badala yake ni kufanya ufisadi ukawa ndiyo mtindo wa maisha.Ujumbe wa aaskofu unasema

vijana wanayo nafasi ndogo ya kuweza kufurahia maisha yao na yenye wema, kinyume chake wanazo fursa nyingi za kutumia madawa ya kulevya , kucheza kamari haramu,nafasi za kufanya ngono na ukahaba, ambavyo uwasababishia kuharibu maisha yao.Imeongeza idadi kubwa ya wasiyo kuwa na ajira kwa asilimia 28,8%,vijana kati yaumri wa miaka 15 na 24 , wakati asilimia 19.7% kuanzia umri wa miaka 15 na 24 hawaendi shule na wala kufanya kazi.Ni hali ya kutisha kwani vijana wanaendelea kijihusisha na vurugu,wizi, mashambulizi, mauaji na kila aina ya uhalifu,wakiongozwa na matumizi hovyo, madawa ya kulevya na mawazo ya kuishi bora ya utajiri rahisi,au kuiga mifano ya wanasiasa wafisadi, wafanya biashara wa madawa ya kulevya Ujumbe unatoa onyo jinsi matumizi mabaya ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii,wakati huo inaongezeka namba kubwa wanao dai hawana dini au kushiriki katika makundi waganga wa kienyeji.Kwa njia hiyo maaskofu wanatoa wito kwamba baada ya kuona hali halisi ya vijana wetu wadogo na wakubwa,tunawakaribisha familia, mamlaka na Kanisa zima kufanya upendeleo wa chaguo moja kwa vijana wetu wadogo na wakubwa.kuwasindikiza katika  maana ya familia, ubora wa elimu hekima msingi ya Biblia , jumuia ya jamii ya kikristo ndivyo vitakuwa muhimu kwa vijana wetu waweze kuwajibika katika kuchukulia maisha kama wito na utume.

Baadaya ya kuweka mtiririko wa mashauri kwa familia, jamii, mamlaka na pia kwa Kanisa zima, wanamalizia maaskofu wakihamasisha vijana kujikita katika jamii ili wawe viongozi wa maisha yao na wito wao,kwa kujikita zaidi katika maadili ya ya Injili , kwa kufuata nyayo za babu zao, ili kutimiza wajibu kiraia , kwa kuheshimu sheria , kwa kutoa heshima ya nchi yao kwa kupitia ishara ya mashujaa , na kuchangia ulinzi wa mazingira, na pia kuwaomba wawe wajasiri wa kuweza kupanga mipango ya ulimwengu endelevu uwe bora. 


Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio

 








All the contents on this site are copyrighted ©.