"Matendo ya kimataifa ya Vatican kwa ajili ya amani" ni kauli mbiu ya Mkutano ambao
Katibu Mkuu wa Sinodi ya maaskofu Kardinali Lorenzo Baldisseri anamehutubia tarehe
24 Frbruari 2017 huko Roveto , ulioandaliwa na Chama cha Kazi ya Kengele wa mashujaa
ambapo mwaka mada inatazama kwa kina juu ya waamuzi.
Kardinali Lorenzo Baldisseri anasema yoyote anayejishughulisha katika kazi ya kidplomasia
anatambua vema ya kwamba bila kuwa na matendo ya kidiplomasia ya Vatican , waamini
wengi na hata wasio kuwa wakatoliki, wanaweza kuona kizingiti katika uhuru wa dini.Na
pia bila uwepo wa vatican katika mikutano mbalimbali ya nchi na kimataifa, kwa hakika
inaweza kuonekana ukosefu wa uzoefu wa ushrikiano wa kibinadamu.Na maneno ya Papa
Paulo wa VI , anasema kwamba matendo ya kuhakikisha kutokuwa na silaha , maelewano
kati ya nchi na vilevile mapambano dhidi ya umasikini na aina zake , vinahitaji ujenzi
kwanza wa amani.
Kwa hayo yote ni utambuzi zaidi kwa wale ambao wanajitoa katika utume wao kama wakleli
katika huduma ya kidplomasia ya Vatican, kwa uwajibikaji ambao unawashirikisha katika
shughuli za utume wa khalifa wa Mtume Petro , kama vile Baba Mtakatifu Francisko analivyosema,
baada ya kukutana na wanadiplomasia septemba 2016 kwamba “katika kazi yenu , mnaitwa
kujikita kila mtu kuleta huduma ya upendo kwa kile mnachowakilisha na kufanya moja
wa kusaidia ulinzi ambao mko tayari kuunga mkono na siyo kusahihisha tu bali tayari
kusikiliza kabla ya kutoa uamuzi , na kufanya hatua ya kuondoa mashaka na mvutano
katika kuleta maelewano.Hayo ni maono wazi ambayo yanasisistizwa kwa upande wa kazi
ya Kanisa ya kidplomasia Vatican, ikiwa inakumbuka na kutazama wazi ule muungano wa
pamoja ulio tolewa na Mtaguo wa Pili wa Vatican katika wosia wa Baba Mtakatifu wa
Mwanga wa mataifa,na kwa upande mwingine ni kuwa sehemu ya miendendo ya hali ya maisha
ya kimataifa , lakini pia kwa mtazamo wa kuangalia lengo kubwa la uwelewa na maridhiano.
Tunaweza kusema kwamba amani ya kweli katika nchi, kama alivyoeleza Mtakatifu Yohane XXIII katika wosia wake wa amani ya katika mataifa (“Pacem in Terris) maana yake ni kutoa ukamilisho wa historia ya wokovu.Hiyo ndiyo kusema kazi ya kidplomasia ya Vatican, maana yake ni kufanya kazi kama chombo cha amani. Katika uvumilivu na subira , kwa kuheshimu kanuni ,katika hali halisi , ambayo haki ya kimataifa inatoa kama msingi wa imani njema.Anaongeza Kardinali Baldisseri ,kuimarisha na kuhakikisha usalama ndiyo inabaki kupewa kipaumbele,na muhimu ili kuzuia sababu za migogoro zinazoweza kurejesha cheche za moto hata kama zilikuwa zimezisitishwa.
Vielelezo vya ukosefu wa haki viko mbele ya macho yetu wote ambapo husababisha hatari
ya amani,kama vile ukiukwaji wa haki,kama vile hukosefu wa chakula, afya,na elimu,ni
baadhi lakini kwa ujumla kwa kuangalia wosia wa Baba Mtakatifu Francisko kuhusu utunzaji
wa mazingira , nyumba ya wote masuala yote yametajwa , kwani tunagutuka kuona ya kwamba
mabadiliko ya tabia nchi inazidi kuwa hatari na kuasababisha maendeleo endelevu yazidi
kuwa mbali katika ulimwengu wetu.
All the contents on this site are copyrighted ©. |