2017-02-23 16:14:00

Mjini Vatican: Toleo jipya la Sheria ya Kiyahudi lazinduliwa


Salam kwenu ninyi mliofika katika tukio la kuzinduliwa kwa toleo jipya ya sheria ya Wayahudi (Torah) na kwa namna ya pekee Rabi Abrahamu Skorka kwa maeno yako na kwa wote mliopata wazo la kuweza kukuunganika mbele ya  sheria hii mpya , kwa maana nyingine ni kusema kuzunguka Bwana na maono yake na  katika neno lake.Ni utangulizi wa maneno ya Baba Mtakatifu Francisko alipokutana na wawakilishi wa kikundi cha wayahudi katika kuzindua toleo Jipya la Sheria ya Kiyahudi.Baba Mtakatifu Francisko anasema Mtakatifu Yohane Paulo  II alielezea Sheria ya Kiyahudi kuwa ni mafundisho ya Mungu aliye hai ambayo yanaoenesha upendo wa kibaba katika uzao wa Mungu.(6,Desemba 1990).  Ni upendo ambao unaundwa na maneno na ishara ya thati,upendo ambao ni agano.

Ni katika neno hili la Agano ambalo limejaa utajiri mkubwa , na kutuunganisha.Mungu ni mkuu na mwaminifu katika Agano lake.Yeye anamwita Abrahamu ili kufanya binadamu wawe kitu kimoja na kuwa na Baraka  kwa watu wote wa dubua, na anaota ulimwengu wa watu waaoungania naye na kuwa na furaha kati tao na viumbe vyote. Mbele ya maneno mengi ya binadamu ambayo kwa bahati mabaya yanasukuma katika mashindano , maeneo matakatifu ya agano , yanafungua njia za wema mahali ambapo tunaweza kukimbilia wote.

Hata toleo hili ni tunda la agano  kati ya watu  wenye utofauti wa utaifa, umri na dini wanaotambua kufanyakazi pamoja.Maridhiano ya kindugu na kanuni kati ya wayahudi na wakristo kwa sasa imehimarishwa na kuwa nzuri , kutokana na kuendeleza kuwa pamoja na ushirikiano.Toleo lenu la leo ni zawadi inayojikita kwa dhati katika maridhiano yenyewa ambayo yanajieleza kwa njia ya maneno  na hata matendo.Sehemu kubwa ya utangulizi wa kitabu maandishi ya mwariri, anaelezea wazi tabia hii ya majadiliano, upeo wa utamaduni ulio wazi na kuheshimiana kwa pamoja  katika amani, uadilifu na ujumbe wa kiroho ndani ya Sheria.

Umuhimu wa watu wa dini ambao wamefanya kazi katika toleo hili jipya, wamejitahidi kwa namana ya pekee kuhifadhi maneno yake,hata kuoensha asili yake, rangi zake ambazo zinatoa thamani ya toleo hilo. Baba Mtakatifu Francisko anamalizia akisema, kila toleo la Maandiko Matakatifu, daima yana thamani ya kiroho ambayo inazidi zaidi ya vifaa.Naomba Mungu abariki watu wote walio shiriki katika kazi hii kwa namna ya pekee ninyi nyote ambapo ninarudia kwa upya shukrani zangu.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.