2017-02-23 17:02:00

Mchakato wa Papa Benedikto wa XIII kuelekea utakatifu wafungwa!


Kardinali Agostini Vallini, Makamu Askofu Jimbo kuu la Roma, Ijumaa tarehe 24 Februari 2017 ameadhimisha ibada maalumu katika Jengo la Kitume Laterano kwa ajili ya kufunga mchakato wa kutangazwa  mwenye heri na mtakatifu, Mtumishi wa Mungu Papa Benedikto XIII. Katika ibada hiyo wameshiriki wahusuka wa mahakama ya Jimbo la Roma walioendesha mchakato mzima , ambao ni Monsinyo Giuseppe D’Alonzo, ambaye ni hakimu, Padre Giorgio Cucci , mhamasishaji wa amani, Marcello Terramani mwandishi wa hati za sheria. Papa Benedikto wa XIII , jina lake la ubatizo ni Pier Francisko Orsini, alizaliwa huko Gravina tarehe 2 Februari 1649 na Ferdinando III mtu wa cheo katika mji wa Gravina , mama yake Giovanna Frangipai akiwa pia mtoto wa Mtu wenye Cheo kikubwa wa Grumo nchini Italia.Papa Benedikto wa XIII alikuwa mtoto wa kwanza kati ya watoto 6, lakini akabaki yatima mapema mara baada ya baba yake kufariki, ambapo yeye akichukua nafasi ya baba yake kuwa mwenye cheo kikubwa cha kuweza kumtumza hata mama yake.

Lakini akiwa bado mdogo alijisikia wito kwa nguvu ndani ya moyo wake , lakini ilibidi aweze kuwa na malumbano ndani ya familia. Baada ya kutaka kujua vema Italia, alikwenda Venezia , mahali amabapo aliweza kukamilisha ndoto yake kwani alipokelewa na Shirika la Wadomenikani, walio kuwa wainjilishaji na kuvaa nguo ya kitawa tarehe 12 Agosti 1668 na kubadili jina la Nugu Vincenzo Maria. Alipata daraja la upadirisho tarehe 24 Februari 1671 na tarehe 22 Februari 1672 akiwa karibu na miaka 22 Papa Clementi XI akamteua kuwa Kardinali.Kwa miaka iliyo fuatia alichukua wadhifa wa kuwa Rais wa Baraza la kipapa la Maridhiano, na kuwa mmojawapo wa baraza mengi hadi alipo changuliwa kwenda kwenye Jimbo Kuu la Manfredonia tarehe 28 Januari 1675 kuwa Askofu Mkuu wa kanisa hilo.

Tarehe 7 Machi 1724 Papa Incocenzo XIII akaga dunia,ndipo wakachangua mfuasi wake ambapo ilihuka muda wa miezi mitatu, Kabla ua Kardinali Vincenzo Maria Orsini akubalia kubadilisja jina lake , na akachaguliwa tarehe 29 Mei 1724.Lakini pamoja na hayo ilibidi kwa nguvu zote abadili hilo jina na ndiyo akachangua jina la Benedikto wa XIII.Kitendo cha kuchaguliwa kuwa papa , akikifanya abadilishe tabia yake aliyokuwa nayo ya kuhudumia kwa unyenyekevu, ubatili wa kiulimwebgu , na hasa zaidi alipendelea wanyonge masikini. Alipunguza hata idadi ya walinzi wake aliokuwa wakimsindikiza kila mara alipotoka na kwenda na kundi dogo wali kuwa wakimsindikiza.Alijishughulisha katika masuala ya kijamii , na hata kwa ajili ya utetezi wa hali halisi ya maisha ya wafungwa m ujenzi wa hiospitali . Pia aliitisha mwaka wa Jubilei 1725 amabapo ilikuwa ni miaka mingi tangu kipindi cha Papa Innocent wa III. Tarehe 21 Februari 1930 akiwa na umri wa miaka 81 , Papa Benedikto wa XIII akaaga dunia. Masalia yake yaliondolewa katika kanisa la Mtakatifu Maria Sopra Minerva tarehe 22 Februari 1733 na  kwa sasa yako katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.